Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani
Mhe Neema Lugangira (MB) akitoa mafunzo ya lishe bora kwa Viongozi wa Dini kutoka mkoa wa Kagera |
Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Mhe Neema Lugangira (MB) akitoa mafunzo ya lishe bora kwa Viongozi wa Dini kutoka mkoa wa Kagera |
Sista Florida Boniface akichangia jambo wakati wa semina hiyo |
Sheikh Adinani akichangia jambo kwenye semina hiyo |
Viongozi wa Dini wa mkoa wa Kagera wakifuatilia kwa umakini semina ya Lishe Bora |
Viongozi wa Dini wa mkoa wa Kagera wakifuatilia kwa umakini semina ya Lishe Bora |
Waratibu wa Kisayansi wakifuatia semina ya Lishe
SHIRIKA la Agri Thamani Foundation limetoa elimu ya Lishe Bora kwa Viongozi wa Dini 124 kutoka Mkoa wa Kagera.
Elimu
hiyo inatolewa na Shirika hilo kwa Viongozi wa Dini ikiwa ni moja ya
vipaumbele vyake kutokana na viongozi hao kuwa na ushawishi mkubwa kwa
jamii.
Akizungumza
wakati wa utoaji wa elimu hiyo Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani
Mhe Neema Lugangira (MB) alisema Viongozi wa Dini wana nafasi kubwa ya
kuchangia kutokomeza udumavu na utapiamlo kwa ujumla nchini kutokana na
nguvu kubwa na ushawishi mkubwa walionao kwa jamii.
Alisema
mwaka jana Agri Thamani ilishiriki katika mchakato wa kuingiza Azimio
la Lishe katika Maazimio ya Viongozi wa Kitaifa kwenye Kifua Kikuu na
Ukimwi.
Aidha
alisema wameanzisha programu ya kutoa Elimu ya Lishe Bora kwa Viongozi
wa Dini Ngazi ya Mkoa, Wilaya na Kata ambapo kwa kuanzia mafunzo hayo
yamepangwa kufanyika mikoa ya Kagera, Kigoma na Tanga na Viongozi wa
Dini kutoka Makundi Yote ya Dini.
Kwa
umoja wao Viongozi hao wa Dini wameishukuru sana Agri Thamani kwa
kupatiwa mafunzo hayo na wamekiri kwamba imewafungua sana na wanakwenda
kuhakikisha ajenda ya Lishe Bora inakuwa ajenda yao ya kudumu na ya
vitendo.
Hata
hivyo wameahidi kufuatilia kwa karibu Utendaji wa Kamati za Lishe za
Ngazi husika ambazo wao kama Viongozi wa Dini wanapaswa kuwa Wajumbe.
Social Plugin