Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WALIOHUSIKA NA UNUNUZI WA MAGARI YA KIFAHARI , CHATO,MSALALA NA KAHAMA WAPEWA SIKU 7

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku saba kuanzia leo (Alhamisi, Desemba 17, 2020) kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, maofisa wanaochambua maombi ya ununuzi wa magari Ofisi ya Waziri Mkuu na wakurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halmashauri ya wilaya ya Chato, Msalala na Kahama wajieleze kwa sababu gani magari hayo yalinunuliwa kwa gharama kubwa.

Ametoa agizo hilo leo Alhamisi, Desemba 17, 2020 wakati akizungumza na watumishi wa umma, Waheshimiwa Wabunge, madiwani katika jiji la Mwanza na Manispaa za Ilemela na Nyamagana katika hoteli ya Malaika, jijini Mwanza. Amesema magari hayo ni mzigo kwa wananchi.

Waziri Mkuu amesema hayo ni matumizi mabaya ya fedha za umma na haiwezekani viongozi hao watumie magari ya gharama kubwa badala ya kutumia fedha hizo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na ametaka muongozo wa ununuzi wa magari uliotolewa na Serikali uzingatiwe.

Amesema matumizi ya fedha za umma lazima yasimamiwe ipasavyo na kwamba Serikali haina mzaha na mtumishi yeyote atakayebainika kutumia vibaya fedha za umma, hivyo amewataka madiwani wakasimamie vizuri maeneo yao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com