Mkurugenzi wa Taasisi ya Furahika Education Tanzania Bw.David Msuya akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi yake leo Jijini Dar es Salaam,
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Wazazi wametakiwa kuwapa nafasi ya masomo watoto wa kike ili kuweza kuwaepusha na vishawishi na kukaa nyumbani kwani wao wanatoa elimu hiyo bure ikiwa dhamira yao kuu ni kuunga mkono Juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Furahika Education Tanzania Bw. David Msuya katika ofisi ya Chuo cha Furahika Education College Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika ofisi hiyo Bw.Msuya amesema katika Chuo chao wamekuwa wakitoa elimu ya Ufundi bure katika nyanja mbalimbali huku mzazi akitakiwa kuchangia Vifaa vya masomo pekee.
“Tunatoa elimu ya Ufundi bure kabisa, lakini mzazi atatakiwa kugharamia vifaa vya masomo, hatupukei fedha ya vifaa bali mzazi atatakiwa kufika navyo vifaa hivyo kama atapoelezwa kwenye fomu”. Amesema Bw.Msuya.
Aidha amewaasa wazazi na walezi kuwapa nafasi ya kuchagua Fani anayoipenda mtoto kusomea ili kukweza kufanikisha ndoto zake ikiwemo kuwapa fursa za kuwapeleka katika vyuo vya ufundi ili kuweza kukabiliana na changamoto za watu kujiari wenyewe.
Vilevile katika fani ya ushonaji wamesema wamekuwa wakitoa zawadi kwa kila muhitimu pindi anapomaliza ambapo hupewa Cherehani moja ili kwenda Kuanzia kazi yake ya ushonaji.
Pamoja na hayo amempongeza Rais Wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa hatua yake ya jana ya kutokutekeleza adhabu ya kifo.
Hata hivyo katika kozi zinazotolewa na Chuo hicho amesema ni pamoja na Ufundi wa kushona, Elimu ya Kompyuta,Upambaji na ususi,Ufundi rangi,Ufundi bomba,Kilimo na kozi nyingine mbalimbali.