Baadhi ya Wazee wakipata chakula cha mchana kwenye halfa hiyo iliyoandaliwa na MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira |
MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara
kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira kushoto akiwa na Mama Muhazi wakifurahia jambo wakati wa halfa hiyo |
MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira (Mb.) amekutana na Wazee 38 waliowakilisha Kata zote 14 za Bukoba Manispaa kwa lengo la hafla fupi ya chakula cha mchana cha pamoja.
Akizungumza wakati akiwakaribisha kwenye hafla hiyo fupi Mhe Neema alisema ameamua kukutana na wazee
hao ambao walifarijika sana huku wakionyesha tabasamu kubwa kutokana na ukarimu ulioonyeshwa na mbunge huyo
Mbunge Neema aliwashukuru wazee
hao kwa namna ambavyo walivyomuunga mkono na kumpa ushirikiano mkubwa
katika cha Kampeni za Kisayansi na m mchango mkubwa uliopelekea
Chama Cha Mapinduzi kupata Ushindi wa Kishindo.
"Kwa kweli niwashukuru sana kwa manufaa ya chama chetu na Taifa kwa ujumla kwa mchango wenu mkubwa na ninaamini ushirikiano huu utakuwa endelevu na wenye tija kwa manufaa ya chama chetu"Alisema
Aidha, Mbunge Neema alisema angependa kutumia fursa hiyo pia kuwapa mrejesho kuhusiana na changamoto za wazee walizowasilisha kwake Kipindi cha Kampeni.
Wakati anawakaribisha kwenye chakula, Mhe Neema Lugangira (Mb.) alitumia fursa hiyo kuwaelezea wazee umuhimu wa Lishe Bora hivyo akawapitisha kwenye menu ya lunch na kila aina ya chakula kina madini na vitamini gani ambazo wanazihitaji zaidi wazee.
“Wazee wangu mnamahitaji maalumu ya Lishe Bora hivyo tutashirikiana pamoja kuona namna bora ya kuhakikisha mnaongeza ulaji wa mbogamboga na matunda” Alisema
Wazee wote walimshukuru sana Mhe Neema Lugangira (Mb) kwa kuwakumbuka na kuwafanya wajiskie wana thamani na walimuomba aendelee na utaratibu aliouanzisha wa kukutana na wazee kuwapa mrejesho wa wanayomtuma na walimshauri kuwa utaratibu huo ufanyike kwa ngazi ya Kata ili aweze kufikia wazee wengi zaidi na kupata uelewa wa kina juu ya mahitaji ya wazee.
Social Plugin