Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza wilayani Chunya leo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akizungumza kulia ni Waziri wa Madini Doto Biteko |
Na, Tito Mselem, Chunya
Waziri
wa Madini Doto Biteko, amefuta Leseni Sita za Wafanyabiashara wa Madini
ya Dhahabu ambao wanatuhumiwa kujishughulisha na utorashaji wa madini
wilayani Chunya.
Watuhumiwa hao, wametakiwa kutojishughulisha na shughuli yoyote ya Madini nchini.
Wakati
huo huo, Waziri Biteko, ameagiza kuondolewa kwa Mwenyekiti wa
wafanyabiashara wa Madini ya dhahabu anaye husika na usimamizi wa Soko
la Madini la Chunya Gagala Poul.
Vile
vile, Waziri Biteko amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Ofisi ya
Madini wa Mkoa wa kimadini wa Chunya baada ya kutuhumiwa kushirikiana na
wafanyabiashara kutorosha madini, ambao watumishi hao ni Gabliel Masai,
Edward Gavana na George Wandiba.
Pia,
Waziri Biteko, ameagiza kusajiliwa kwa Mialo yate inayo chenjua madini
ya dhahabu wilayani Chunya ili kujua mwalo gani umezalisha kiasi gani
cha dhahabu na dhahabu hiyo imepelekwa kuuzwa soko gani.
“
Bora tubaki na wanunuzi wawili wa madini ya dhahabu ambao ni waanifu
kuliko kuwa na mlolongo wa wanunuzi ambao sio waaminifu na wasio fuata
kanuni, taratibu na sheria zilizowekwa,” amesema Waziri Biteko.
Waziri
Biteko amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila
kuwapa zawadi wale wote watakao saidia kupatikana kwa watu wanao torosha
madini.
“Niwaombe
wachimbaji na wafanyabiashara wote wa madini kutoa ushirikiano kwa
Serikali ili kukomesha tatizo la utoroshaji madini, tunataka nidhamu
kwenye sekta ya madini ili tulete tija na maendeleo nchini,” amesema
Waziri Biteko.
Pia,
Waziri Biteko, amewataka wachimbaji na wafanyabiashara wote wa madini
nchini kuhakikisha wanapeleka madini yao sokoni na kuachana na
ufanyajibiiashara ya madini nje ya masoko ya madini.
Naye,
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amepongoza Waziri wa Madini kwa
kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bukombe na kuteuliwa tena kuwa Waziri wa
Madini.
Pia, Chalamila
amesema Serikali imeshaanza kujenga gereza ili watu watakao kamatwab
wakitorosha madini hawatapekwa mbeya mjini bali watafungwa katika gereza
hilo.