WAZIRI CHAMURIHO AWATAKA WAFANYAKAZI KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho amewataka watumishi wa wizara Ujenzi na Uchukuzi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi ili kuongeza ufanisi. 


Akizungumza na menejimenti ya Sekta ya Ujenzi na Uchukuzi mara baada ya kuwasili ofisini hapo jijini Dodoma ameitaka menejimneti kuunganisha wafanyakazi wa sekta zote kufanya kazi kwa kuzingatia matokeo yanayopimika.


“Jipangeni kuhakikisha kuwa Watumishi wote wanafanya kazi kwa umoja na ushirikiano ili kufikia malengo yanayotarajiwa na Serikali katika kuboresha miundombinu nchini’ amesema Eng. Dkt. Chamuriho.


Amemtaka Katibu Mkuu-Ujenzi Arch. Elius Mwakalinga na Kaimu Katibu Mkuu Uchukuzi Gabriel Migire kuhakikisha miradi yote inayoendelea ujenzi wake unakamilika kwa wakati na tija.

 
Kwa upande wake Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Eng. Godfrey Kasekenya ameitaka menejimenti ya Wizara kuweka ratiba ya mara kwa mara ya kukagua miradi ili kupata taarifa ya maendeleo na kuchukua hatua mapema kwa miradi yenye changamoto. 


Akiwakaribisha Waziri na Naibu Waziri, Katibu Mkuu Ujenzi amewahakikishia viongozi hao ushirikiano kati yao menejimenti na watumishi kwa sekta anazosimamia.


Waziri Eng. Dkt. Leonard Chamuriho na Naibu Waziri Eng. Godfrey Kasekenya walikuwa katika kikao cha kwanza cha na menejimenti ya wizara mara baada  ya kuteueliwa kuongoza wizara hiyo hivi karibini.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post