Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BENKI YA ABSA YAKABIDHI VIFAA VYA USAFI KWA SHULE 54

Na Fred Alfred - Dodoma
BENKI ya ABSA imetoa vifaa vya usafi kwa shule 54 za halmashauli ya jiji la Dodoma vyenye thamani ya Sh. milioni 10 vitakavyotumiwa na wanafunzi kujiweka safi wanapokuwa shuleni.

Akizindua vifaa hivyo mwakilishi wa mkurugenzi wa jiji la Dodoma Elias Mazengo alisema vifaa  vilivyotolewa na benki hiyo  ni pamoja na ndoo 304 na sabuni ambazo zitaanza kugawiwa hivi karibuni kwa shule zote lengwa.

Alisema vifaa hivyo vitasaidia wanafunzi kunawia mikono baada na kabla ya kula chakula chochote itasaidia kupunguza magonjwa mlipuko.

“Tunashukuru wadau wetu Benki ya ABSA  kwa kutuletea msaada huu, utasaidia kupunguza magonjwa ya mlipuko kwa wanafunzi na kuwajengea utamaduni wa kunawa mikono mara kwa mara”,alisema.

Kwa upande wake Muwakilishi wa Benki ya ABSA Elizabeth Kiwale alisema lengo la kutoa msaada huo ni kuhakikisha wanafunzi wanalindwa afya zao wanapokuwa shuleni.

Alisema Benki ya ABSA  inashirikiana na serikali kuhakikisha wanaisaidia jamii katika masuala mbalimbali na hiyo ni kama shukrani kwasababu wateja wake wakubwa wanatoka katika jamii.

“Tunatambua mchango wa jamii kwenye benki yetu na leo tumeamua kutoa misaada hii ilivijana wetu wanapokuwa shule afya zao zikawe stimilifu, na vifaa hivi vitawasaidia kunawa mikono mara kwa mara ilikujiepusha na magonjwa ya mlipuko”,alisema.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya wakuu wa shule Mkuu wa Shule ya Ipagala B Praxeda Fundisha alisema vifaa hivyo vitasaidia kupunguza magonjwa ya mlipuko kwa wanafunzi ambayo yanasababishwa na uchafu.

Alisema  kwa upandew wa wanafunzi hasa wa shule za msingi ni haki ya mzazi na mwalimu kumlinda afya yake kuhakikisha anakuwa katika mazingira bora sambamba na kuipongeza Benki ya ABSA kwa kutambua afya za watoto.

“Tunawashukuru sana absa kwa kutambua mchango wa afya za watoto kupitia misaada hii itasaidia kupunguza magonjwa ya mlipuko ambayo kipindi cha nyuma yalikuwa ni tishio hasa kwa watoto wa shule za misingi ambao kwa kiasi kikubwa inabidi tuwalinde”alieleza

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com