Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC NCHIMBI AAGIZA TAKUKURU KUWASAKA MAWAKILI NA MAHAKIMU UMIZA MITAANI “BUSH LAWYERS”

 

Mkuu waMkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akihutubia kwenye sherehe zamaadhimisho ya uzinduzi wa wiki ya sheria, kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Kiomboi juzi.
Nchimbi akiwa na viongozi mbalimbali wa mahakama na serikali kwenye maadhimisho hayo
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Luhaula akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Dkt Rehema Nchimbi akihutubia kwenye sherehe za maadhimisho ya uzinduzi wa wiki ya sheria mwaka huu, kwenye viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida.
Mkuu wa Mkoa akitembelea moja ya banda la wadau wa mahakama linalojishughulisha na kazi za usaidizi wa msaada wa kisheria wilaya ya Singida.
Akiwa kwenyebanda la Jeshi la Magereza.
Akiwa kwenye banda la Watumishi wa Mahakama.
Baadhi ya Watumishi na Mahakimu wa Wilaya ya Iramba wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzihuo
Wananchi kutoka Taasisi na Asasi mbalimbali wakishiriki maadhimisho hayo
Mada mbalimbali zikiwasilishwa.

Sherehe zauzinduzi zikiendelea.

Na Godwin Myovela, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi ameiagizaTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuanza mara moja msako wa kuwabaini na kuwachukulia hatua Mawakili na Mahakimu Umiza walioko mitaani maarufu‘Bush Lawyers’ ambao wamekuwa kikwazo kwa kushawishi, kuwatoza tozo kubwa na kuwavuruga raia ili wakatae, wakinzane au kutokukubaliana na mienendo halali ya kesi zinazoamriwa na mahakama kwa mujibu washeria.

Nchimbi alitoa agizo hilo kwa nyakati tofauti wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya sheria kwa Wilaya za Iramba na Singida juzi, huku akisisitiza kwa kuwataka Takukuru kuanza kuwatafuta na kuwashughulikia watu hao kwa mujibu wa sheria kama walivyofanikiwa kudhibiti Wakopeshaji Haramu.

“Haiwezekani hata kidogo tukaendelea kufumbia macho jambo hili. Hawa mawakili umizana mahakimu uchwara huko mtaani wanaumiza sanawatu…wanawadanganya na wakati mwingine kusababisha mienendo ya kesi kubadilika mara kwa mara, hawa ni wavurugaji wakubwa wa mashauri!” alisema Mkuu wa Mkoa.

Akitoa tafakuri na tathmini juu ya maadhimisho hayo kuelekea kilele cha siku ya sheria mwaka huu, na mantiki ya umri wa miaka 100 ya mahakama katika muktadha wa uwiano wa haki nchini, Nchimbi alianza kwa kusema miaka hiyo ni faraja, ni sherehe na ni kitu cha kujivunia.

Alisema kwenye michezo ya  burudani siku zote mashabiki wananafasi kubwa ya kucheza wakiwa nje ya uwanja kuliko hata wachezaji wenyewe, na wakati mwingine mashabiki hao hao wanasahau kwamba jukumu la timu linawahusu na wao pia, wanafikiri wapo nje ya uwanja hapana!..na wao wapo ndani.

Nchimbi alisema asili ya sheria ni Mungu mwenyewe. Au kwa maana nyingine Mungu ni Sheria. Kama mwanadamu atamtii Mungu basi atazitii, atazifahamu, atazipenda, atazienzi, ataziheshimu na kuziishi sheria.

Alisema kila kilichoumbwa kwa sura na mfano wa Mwenyezi Mungu hapa duniani kimeumbwa kwa kufuata sheria. 

Mkulima hawezi kustawisha mazao na kupata mavuno mengi kama atavunjasheria. 

Mfugaji hawezi kumudu kufuga ipasavyo bila kufuata sheria, mvuvi vile vile na kadhalika. 

Viungo vyote vya mwili macho, moyo, utumbo, masikio, miguu na kila kitu kimewekwa na kipo pale kwa mujibu washeria.

Aliwahamasisha Watendaji wa Mahakama kuongeza kasi ya kutoa elimu ili jamii ijue na kuzingatia sheria kwa ustawi wa haki na wajibu. 

“Pia watu wafahamishwe kuwa haya mambo ya kesi hayana shortcut (njiazamkato) nilazima jamii izingatie utii wa sheria bila shuruti kwa faida ya wewe, yule na mimi-kiusalama na kwa ustawi wa maendeleo.”

“Ikiwezekana hata Jeshi la Magereza nalo natamani siku moja livunje ule ukuta wa gereza kwa kuwachukua na kuwapeleka wafungwa hao wakiwa hivyo hivyo na sare zao kuchanganyikana na raia kwenye makanisa, misikiti na mashuleni ili watu na jamii ione kwa macho, iguswe na kujifunza madhara ya kubaka, kulawiti, kuiba, rushwa na aina nyingine ya makosa endapo mtu atavunja sheria,” alisema

 

Nchimbi alisema mahakama au kutimiza miaka 100 bado haitoshi kama watu hawatazipenda, hawata zingatia na kuziishi sheria. 

Ifike mahali tujiulize mathalani hata unapoajiriwa au kujiajiri ili kila jambo liende sawa sawa na kwa utaratibu mzuri ni lazima mahali hapo pawekwe sheria. Miaka hii100 itutafakarishe na kutuongoza kutathmini  kama taifa kwanini sheria? inamhusunani? na kwanini miaka 100 ya kutafsiri sheria? 

Na kwa muktadha huo, mchango wa mahakama katika Ustawi wa Tanzania ya amani, uhuru, udugu, demokrasia bora, utawala wa sheria, ustawi wa uchumi utaonekana kudhihirika…na mashabiki walio nje ya uwanja wataunga na nawachezaji, sote tutajiona tupo ndani ya uwanja, tutajiona ni sehemu ya mchezo husika, na tutazingatia.

Maadhimisho ya wiki ya sheria mpaka sasa yanaendelea kwenye maeneo mbalimbali katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Singida kwa kwa watumishi na wadau mbalimbali wa mahakama kutoa elimu na huduma za msaada wa kisheria, sambamba na kutathmini kwa pamoja dhima kuu ya mwaka huu isemayo“Miaka 100 ya Mahakama Kuu: Mchango wa Mahakama katika kujenga nchi inayozingatia uhuru, udugu, amani na ustawi wa wananchi.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com