Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS MAGUFULI AZINDUA MRADI WA MAJI ISAKA- KAGONGWA ...AMPONGEZA AWESO KUFUKUZA WAKANDARASI FEKI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungulia maji kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika mji mdogo wa Kagongwa na Isaka leo tarehe 29 Januari 2021 katika eneo la Kagongwa, Kahama mkoani Shinyanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishika maji mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika mji mdogo wa Kagongwa na Isaka leo tarehe 29 Januari 2021 katika eneo la Kagongwa, Kahama mkoani Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungulia maji kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika mji mdogo wa Kagongwa na Isaka leo tarehe 29 Januari 2021 katika eneo la Kagongwa, Kahama mkoani Shinyanga.
Sehemu ya Matanki ya kusambazia maji katika mradi huo wa maji Kagongwa -Isaka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuzindua upanuzi wa Mtandao wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika mji mdogo wa Kagongwa na Isaka Kahama mkoani Shinyanga leo tarehe 29 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Meneja mradi Mhandisi Felister Lyimo kuhusu mradi wa maji wa Isaka-Kagongwa kabla ya kuzindua mradi huo wa maji mkoani Shinyanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kagongwa mkoani Shinyanga mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji. 

Picha na Ikulu
****
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, amempongeza Waziri wa Maji Jumaa Aweso kwa kuchukua maamuzi ya kuwafukuza wakandarasi feki wa mradi wa maji uliopo Mwanga na kumweleza kuwa kama angechelewa basi angemfukuza yeye.

Rais Magufuli ameitoa kauli hiyo leo Ijumaa Januari 29, 2021, wakati akizindua mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria wa Kagongwa hadi Isaka mkoani Shinyanga huku , ambapo akiwataka viongozi wahakikishe miradi yote wanayoisimamia haikwami na ikiwezekana ikamilike kabla ya muda.

"Watanzania wamechoka kusubiri miradi, nataka miradi ikamilike mapema na isiwe inazaa variation, nimeshukuru umeanza kuchukua hatua kwa wakandarasi feki waliokuwa kule Mwanga ukawafukuza kwa sababu ungechelewa kuwafukuza mimi ningekufukuza wewe ni vizuri wale wanaokuchelewesha wewe fukuza tu", amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Maji Jumaa Aweso kupeleka majina ya wakandarasi walioshindwa kukamilisha miradi ya maji nchini katika bodi ya usajili wa wakandarasi ili wafutwe na wasipewe kazi ndani ya nchini na nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika ya Mashariki.

"Pia wale wakandarasi uliowafukuza, zungumza na bodi ya wakandarasi wafutwe na wasipate kazi yoyote Tanzania kwa vile tuna ushirikiano wa Nchi za Jumuiya ya Umoja wa Afrika Mashariki peleka majina yao kule hatuhitaji wakandarasi matapeli, Waziri umeanza vizuri na moto ulioanza nao endelea nao, usicheke na hawa wakandarasi cheka na maji unapokuwa unayanywa", ameongeza Rais Magufuli.

Mradi huo wa maji wa Kagongwa – Isaka uliotakiwa kutumia shilingi Bilioni 24, umejengwakwa gharama ya shilingi bilioni 23.1 na utasaidia kutatua changamoto ya uhaba wa maji kwa wananchi wa maeneo hayo.

Aidha Rais Magufuli ameagiza shilingi bilioni 1.5 zilizobaki katika mradi huo zitumike kusambaza maji katika vijiji vinavyozunguka mradi huo.

“Fedha za kutekeleza mradi huu zimetokana na kodi za wananchi. Nawapongeza Watanzania kwa kuwezesha kutekeleza mradi huu kwani wananchi walikuwa na uhitaji wa maji. Tutashirikiana kwa pamoja kujenga uchumi wenye kuleta maendeleo ya wananchi”, amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema amemuomba radhi Mhe. Rais Magufuli kwa miradi ambayo imekwamishwa na wakandarasi na kuahidi kuikamilisha haraka iwezekanavyo.

Kuzinduliwa kwa mradi huo wa maji kutasaidia kupunguza adha ya maji kwenye maeneo ya Kagongwa na Isaka ambapo sasa wataweza kupata maji safi na salama na kutumia maji hayo katika matumizi mengine.
 
Soma pia:

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com