Frank Lampard ameshinda michezo 28 kati ya 57 aliyoiongoza Chelsea katika Ligi ya Primia.Lampard (42), ambaye ni kuingo wa zamani wa klabu hiyo, anaiacha Chelsea katika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi ya Primia huku wakishinda mechi moja tu ya ligi kati ya tano zilizopita. Mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu wiki iliyopita walifungwa na Leicester City.Mechi yake ya mwisho kama kocha wa miamba hiyo ya London ulikuwa Jumapili wakishinda 3-1 dhidi ya Luton kwenye michuano ya FA.Kocha wa zamani wa Paris St-Germain na Borussia Dortmund Thomas Tuchel anatarajiwa kutua katika dimba la Stamford Bridge kurithi nafasi ya Lampard.Lampard amekuwa kocha wa 10 kuajiriwa na Roman Abramovich tangu tajiri huyo alipoinunua Chelzea mwaka 2003. Aliajiriwa mwaka 2019 kwa mkataba wa miaka mitatu kuchukua nafasi ya Maurizio Sarri.Inakadiriwa kuwa Abramovich ameshatumia pauni milioni 110 kuwalipa makocha aliowatimua kazi kabla ya Lampard.Katika kipindi chote cha umiliki wa Abramovich, Lampard ni kocha wa pili kuwa na uwiano mbovu wa matokeo wa asilimia 52.4, ni Andre Villas-Boas (47.5%) ambaye mwenye uwiano mbovu zaidi.Uwiano wa wa ushindi wa Jose Mourinho alipoinoa klabu hiyo mara ya kwanza ulikuwa 67.03%, wakati while Antonio Conte, Maurizio Sarri, Avram Grant, Carlo Ancelotti na Claudio Ranieri wote wakiwa na zaidi ya 60%.
CHANZO - BBC SWAHILI
Social Plugin