Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SHIRIKA LA RAFIKI SDO LACHANGIA MIFUKO YA SARUJI UJENZI WA MADARASA MAZINGE SEKONDARI

Kulia ni Meneja Miradi wa Shirika la Rafiki SDO, Dk. Nyamkongi Lucas akimkabidhi mifuko ya saruji Afisa Mtendaji wa Kata ya Ndembezi, Timothy Timoth kwa ajili ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mazinge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Rafiki Social Development Organization (Rafiki SDO) limechangia mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili kwenye shule ya Sekondari Mazinge iliyopo katika Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga. 

Meneja Miradi wa Shirika la Rafiki SDO, Dk. Nyamkongi Lucas amekabidhi mifuko ya saruji yenye thamani ya shilingi 190,000/= leo Jumatano Januari 6,2021 kwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Ndembezi, Timothy Timoth katika shule ya Sekondari Mazinge. 

Dk. Lucas amesema Shirika la Rafiki SDO limetoa msaada huo wa mifuko ya saruji kutokana na kwamba wao ni wadau wa maendeleo hivyo wameguswa ili kufanikisha zoezi la ujenzi wa madarasa kwa sababu linawahusu watu wote katika jamii. 

“Tunahitaji kujenga jamii yenye watu wasomi, hivyo hatuwezi kupata wasomi kama hatujawatengeneza sisi wenyewe. Ni sisi wanajamii tunahusika katika kujenga wasomi hawa hivyo kama sehemu ya jamii tumechangia mifuko 10 ya saruji yenye thamani ya shilingi 190,000/= kuongeza nguvu katika ujenzi wa madarasa”,amesema Dk. Lucas. 

“Tutazidi kushirikiana na serikali katika shughuli za maendeleo kwa sababu sisi jina letu ni Rafiki Social Development Organization kwa hiyo maendeleo ya jamii ni sehemu yetu. Tunapoona jamii inafanya maendeleo sisi kama wadau wakuu wa maendeleo tunawiwa zaidi kushirikiana nao”,ameongeza Dk. Lucas 

Akipokea mifuko hiyo ya saruji, Afisa Mtendaji wa kata ya Ndembezi Timothy Timoth amelishukuru Shirika la Rafiki SDO kwa mchango huo wa mifuko ya saruji akieleza kuwa itasaidia katika kumalizia ujenzi wa madarasa 

Aidha Timoth amewaomba wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kwani jambo la ujenzi wa madarasa ni la watu wote katika jamii. 

Amesema shule ya Sekondari Mazinge ina uhitaji wa madarasa manne hivi sasa wanaendelea na ujenzi wa madarasa mawili unaotarajiwa kukamilika Januari 10,2021 huku akibainisha kuwa jumla ya wanafunzi 230 kuanza masomo ya kidato cha kwanza tofauti na mwaka 2020 ambapo wanafunzi walikuwa 196. 
Kulia ni Meneja Miradi wa Shirika la Rafiki SDO, Dk. Nyamkongi Lucas akimkabidhi mifuko ya saruji Afisa Mtendaji wa Kata ya Ndembezi, Timothy Timoth kwa ajili ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mazinge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga leo Jumatano Januari 6,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Kulia ni Meneja Miradi wa Shirika la Rafiki SDO, Dk. Nyamkongi Lucas akimkabidhi mifuko ya saruji Afisa Mtendaji wa Kata ya Ndembezi, Timothy Timoth kwa ajili ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mazinge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mifuko ya saruji iliyotolewa na Shirika la Rafiki SDO kwa ajili ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mazinge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Kulia ni Meneja Miradi wa Shirika la Rafiki SDO, Dk. Nyamkongi Lucas akizungumza wakati akikabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mazinge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni  Afisa Mtendaji wa Kata ya Ndembezi, Timothy Timoth akilishukuru Shirika la Rafiki SDO kwa kuchangia mifuko ya saruji kwa ajili ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mazinge.
Wadau wa maendeleo wakiwa katika eneo la ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mazinge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga. 
Wadau wa maendeleo wakiwa katika eneo la ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mazinge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com