Brigedia Jenerali mstaafu, Emmanuel Maganga enzi za uhai wake.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu, Emmanuel Maganga amefariki dunia leo Alhamis usiku Januari 21,2021.
Taarifa za awali zinasema kuwa Brigedia Jenerali mstaafu, Emmanuel Maganga amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Jeshi mkoani Tabora.
Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga alistaafu mwezi Julai, mwaka 2020 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Bw. Thobias Andengenye (aliyewahi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji) kuwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma kuchukua nafasi ya Brig. Gen. (Rtd) Emmanuel Maganga.
BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
Social Plugin