NAIBU WAZIRI SILINDE AZIAGIZA HALMASHAURI KUHAKIKISHA WANAFUNZI WOTE WANAKAA KWENYE MADAWATI DARASANI


Naibu Waziri wa TAMISEMI David Silinde ameagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekaa chini kwa kukosa madawati au kusoma chini ya miti kwa upungufu wa madarasa na kuagiza ujenzi wa madarasa katika wilaya zote uanze mara moja kwa yale maeneo yenye upungufu wa madarasa.

Hayo ameyasema alipotembelea shule ya msingi King'ongo iliyopo wilaya ya Ubungo mkoa wa Dar es salaam kufuatia agizo la Rais wa Tanzania Dr. John Magufuli la kutaka ujenzi wa madarasa hayo ukamilike kwa haraka.

Naibu Waziri Silinde amesema serikali ilitoa fedha kwa ajili ya ujenziwa madarasa maeneo mengi ya nchi katika mradi wa lipa kwa matokeo EP4R tangu mwezi wa Sita mwaka jana lakini madarasa bado hayajakamilika katika baadhi ya maeneo lakini ujenzi wa madarasa katika shule ya King'ongo yanakamilika kwa wiki zisizozidi tatu na kutaka watendaji katika wilaya zote kukamilisha ujenzi bila kusukumwa na viongozi wakubwa wa nchi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic amemwambia Naibu waziri wa TAMISEMI kuwa ujenzi wa madarasa huo utakamilika tarehe 31 mwezi huu na mpaka tarehe tano wanafunzi wataanza kuyatumia madarasa hayo na mpaka kukamilika yatatumia zaidi ya milion 205 ujenzi wa vyumba tisa ambavyo vitakua na madawati yake pamoja ujenzi wa choo chenye matundu 12.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post