Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU YALIPA USHURU BIL 2.3 KWA AJILI YA MAENDELEO MANISPAA YA KAHAMA NA HALMASHAURI YA MSALALA

Viongozi wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na Manispaa ya Kahama,halmashauri ya Msalala na Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (wa tatu kushoto) baada ya makabidhiano ya hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 2.387 kwa Manispaa ya Kahama na Halmashauri ya wilaya ya Msalala ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma ‘Service Levy’

 Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Twiga Minerals kupitia Migodi yake ya Buzwagi na Bulyanhulu imekabidhi hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 2.387 ( Tsh. 2,387,745,061.23/=) kwa Manispaa ya Kahama na Halmashauri ya wilaya ya Msalala ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma ‘Service Levy’ kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2020.

Hafla fupi ya makabidhiano imefanyika leo Jumamosi Januari 30, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Kahama na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na viongozi wa Manispaa ya Kahama na halmashauri ya Msalala wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha.

Akikabidhi hundi hizo, Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi,Benedict Busunzu amesema mgodi wa Buzwagi umelipa kiasi cha shilingi 1,642,815,335.45/= kwa Manispaa ya Kahama huku Mgodi wa Bulyanhulu ukilipa shilingi 744,929,725.78/= ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo.

“Kampuni ya Twiga Minerals ambayo ni Kampuni inayoundwa ka ushirikiano baina ya Kampuni ya madini ya Barrick na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia migodi yake ya Buzwagi na Bulyanhulu leo tunakabidhi jumla ya shilingi Bilioni 2.387 kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika Manispaa ya Kahama na halmashauri ya Msalala”,amesema Busunzu.

“Tunapokabidhi fedha hizi tunaona Fahari kubwa kwa kuwa tunaendelea kuona matunda ya matumizi sahihi ya fedha hizi katika uboreshaji wa  miundo miundombinu mbalimbali inayoimarisha uchumi na huduma muhimu kwa ajili ya wananchi”,ameeleza Buzunzu.

Busunzu amesema Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu inafurahi kuwa sehemu ya mafanikio ya maendeleo ya Kahama na Msalala na mkoa wa Shinyanga kwa ujumla aambapo kipimo  cha mafanikio hayo ni matokeo chanya na endelevu yanayotokana na mchango wa fedha ambazo wamekuwa wakitoa.

“Tumeshuhudia mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupadishwa hadhi Halmashauri ya Mji wa Kahama kuwa Manispaa ya Kahama.Tunapenda kuwapongeza sana viongozi wetu wa serikali na wananchi kuanzia ngazi ya kijiji tunakochimbia madini hadi mkoa kwa ushirikiano na juhudi tunazoziona za kusimamia vizuri matumizi ya fedha za ushuru wa huduma ambazo tunalipa kila baada ya miezi sita”,ameongeza Busunzu.

“Juhudi hizo zinatuhamasisha kufanya kazi zaidi ili tuzalishe zaidi na tulipe ushuru mkubwa na kuendelea kuchangia zaidi maendeleo chanya katika Manispaa ya Kahama,halmashauri ya Msalala na mkoa wa Shinyanga kwa ujumla",amesema Busunzu.

Amesema Kampuni ya Twiga Minerals kwa kushirikiana na serikali na wadau wengine wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi itaendelea kujenga jamii endelevu ili kuendana na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Dira ya Taifa 2025.

Akipokea Hundi hizo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha ameishukuru Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu kwa kulipa ushuru wa huduma kwa wakati na hivyo kuongeza mapato ya ndani ya Manispaa ya Kahama na halmashauri ya Msalala akibainisha kuwa fedha hizo kiasi cha shilingi Bilioni 2.3 zitatumika kwa ajili ya mahitaji ya wananchi.

“Migodi hii inatusaidia sana kupata fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo na imekuwa na mchango mkubwa sana katika kuifanya Halmashauri ya Mji wa Kahama ipandishwe hadhi na kuwa Manispaa ya Kahama”,amesema Macha.

Mkuu huyo wa wilaya ya Kahama amewaelekeza Wakurugenzi wa Manispaa ya Kahama na halmashauri ya Msalal kutumia fedha katika sekta ya elimu na afya ili kuondokana na changamoto zilizopo kwenye baadhi ya maeneo.

Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, Benedict Busunzu (wa tatu kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha ( wa pili kushoto) hundi ya shilingi 744,929,725.78  kwa ajili ya Halmashauri ya Msalala ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo leo Jumamosi Januari 30,2021. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi,Benedict Busunzu (wa tatu kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha ( wa pili kushoto) hundi ya shilingi 744,929,725.78  kwa ajili ya Halmashauri ya Msalala ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha ( wa pili kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege hundi ya shilingi 744,929,725.78 zilizotolewa na mgodi wa Bulyanhulu kwa ajili ya Halmashauri ya Msalala ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha ( wa pili kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege hundi ya shilingi 744,929,725.78 zilizotolewa na mgodi wa Bulyanhulu kwa ajili ya Halmashauri ya Msalala ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, Benedict Busunzu (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (wa tatu kushoto) hundi ya shilingi 1,642,815,335.45/=  kwa ajili ya Manispaa ya Kahama ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Anderson Msumba, akifuatiwa na Meya wa Manispaa ya Kahama, Yahaya Ramadhani Bundala.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, Benedict Busunzu (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (wa tatu kushoto) hundi ya shilingi 1,642,815,335.45/=  kwa ajili ya Manispaa ya Kahama ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo.
Meya wa Manispaa ya Kahama, Yahaya Ramadhani Bundala akimkabidhi Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Anderson Msumba hundi ya shilingi 1,642,815,335.45/= zilizotolewa na mgodi wa Buzwagi kwa ajili ya Manispaa ya Kahama ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, Benedict Busunzu akizungumza wakati akikabidhi hundi za shilingi Bilioni 2.3 ambapo amesema mgodi wa Buzwagi umelipa kiasi cha shilingi 1,642,815,335.45/= kwa Manispaa ya Kahama huku Mgodi wa Bulyanhulu ukilipa shilingi 744,929,725.78 ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akiushukuru mgodi wa Buzwagi kwa kulipa kiasi cha shilingi 1,642,815,335.45/= kwa Manispaa ya Kahama na Mgodi wa Bulyanhulu kulipa shilingi 744,929,725.78 ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo.
Meya wa Manispaa ya Kahama, Yahaya Ramadhani Bundala akiishukuru Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu kwa kuendelea kutoa ushuru wa huduma kwa wakati na kuahidi kutumia fedha zilizotolewa kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Viongozi wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na Manispaa ya Kahama,halmashauri ya Msalala na Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (wa tatu kushoto) baada ya makabidhiano ya hundi hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 2.387 kwa Manispaa ya Kahama na Halmashauri ya wilaya ya Msalala ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma ‘Service Levy’
Viongozi wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na Manispaa ya Kahama,halmashauri ya Msalala na Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (wa tatu kushoto) baada ya makabidhiano ya hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 2.387 kwa Manispaa ya Kahama na Halmashauri ya wilaya ya Msalala ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma ‘Service Levy’
Viongozi wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na Manispaa ya Kahama,halmashauri ya Msalala na Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (wa tatu kushoto) baada ya makabidhiano ya hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 2.387 kwa Manispaa ya Kahama na Halmashauri ya wilaya ya Msalala ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma ‘Service Levy’
Muonekano hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 2.387 kwa Manispaa ya Kahama na Halmashauri ya wilaya ya Msalala zilizotolewa na Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma ‘Service Levy’
Muonekano wa Hundi ya shilingi 744,929,725.78/= ambazo zimetolewa na Mgodi wa Bulyanhulu kama ushuru wa malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo.
Muonekano wa hundi ya shilingi 1,642,815,335.45/= iliyotolewa na mgodi wa Buzwagi kwa Manispaa ya Kahamaambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com