Kwa Mujibu wa gazeti la The Telegraph la Uingereza jamaa huyo alikuwa amewaficha wanyama hao katika soksi na masanduku ya barafu alipokamatwa na maofisa forodha wa uwanja huo wa Vienna.
Naibu katibu mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania, Allan Kijazi amesema mwanaume huyo alisafiri kwenda Austria kutoka Tanzania kupitia Ethiopia na kwamba mujibu wa gazeti hilo vinyonga hao walikuwa wakipelekwa kwenye bustani ya wanyama ya Schoenbrunn na ilibainika kuwa watatu wamekufa.
Amesema wanyama wote walikuwa wanatoka katika milima ya Usambara Tanzania na walikuwa katika umri wa wiki moja hadi wakubwa ambao walitakiwa kuuzwa katika masoko ya ulanguzi.
Social Plugin