Taarifa kuhusu chama cha wanaume wachoyo cha Nigeria- Stingy Men Association of Nigeria (Smen), imeenea kwenye mtandao wa kijamii waTwitter nchini Nigeria huku wanaume maarufu wa Nigeria wakishirikisha umma kadi za uanachama wao wa kikundi hicho.
Ujumbe wa Twitter wa mzalishaji wa muziki Don Jazzy wa kadi yake ya uanachama ulishirikishwa tena na wafuasi wake mara 11,000.
Nyota wa muziki wa Afrobeats Bw Eazi pia alituma kati yake ya uanachama katika chama cha wanaume wachoyokupitia mtandao wa Twitter.
Akaunti rasmi ya chama cha wanaume wachoyo kwenye mtandao wa Twitter ilionekana kwenye mtandao huo kwa mara ya kwanza Jumatatu.
Wanaotuma jumbe za Twitter wamekuwa wakitania kuwa watabuni wimbo wao maalumu, makao makuu na kiapo.
Haijawa wazi ni vipi taarifa ya chama cha wanaume wachoyo iliyoshirikishwa zaidi kwenye Twitter ilivyoanza nchini Nigeria. Wazo hilo tayari limesambaa katika mataifa mengine ya Afrika.
Mwezi Disemba taarifa ya gazeti la Uganda la Daily Monitor iliainisha pendekezo la kikundi hicho nchini Uganda.
Katika taarifa hiyo iliyoandikwa na , Ian Ortega aliandika: "Katiba hii iliandikwa katika mwaka wa janga la corona itaelezea maana ya hatua kali ."
Sehemu ya"katiba yake " iliwalenga marafiki wa kike wanaowaomba wapenzi wako wa kiume pesa.
"Kila binti wa Eva ambaye anaomba pesa atachukuliwa kama muhamiaji haramu na kuepukwa; ‘hafai kuwa mke ,’" aliandika.
Aliendelea kusema kuwa “mjumbe hapaswi kuhisi aibu yoyote katika kukataa ombi lolote la pesa linalowasilishwa kwake.”
Hii ni pamoja na maombi ya pesa za usafiri au salio la simu.