Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa
**
Serikali imesema inatambua mchango wa sekta ya habari na kuahidi kuzishughulikia changamoto za tasnia hiyo kwa kufanya maboresho, kupitia sheria na mikutano na wanahabari.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dae es Salaam, Januari 9, 2021.
Baadhi ya changamoto zilizoibuliwa na waandishi wa habari ni pamoja na waandishi kukosa mikataba ya kudumu ya kazi, kufanya kazi kwa kujitolea kwa muda mrefu, bei kubwa ya kusajili ' Blogs na Online TV', wasemaji wa taasisi za serikali kutotoa ushirikiano katika masuala yanayohitaji ufafanuzi kwa kero za jamii na wavamiaji wa taaluma.
Akizijibu changamoto hizo, Waziri Bashungwa amesema atashirikiana na wizara nyingine ikiwemo ya kazi ili kutatua suala la ajira kwa wanahabari.
''Suala hili la ajira kwa mujibu wa sheria kama lilikua halisimamiwi, basi nitashirikiana na Wizara ya Ajira kuhakikisha waandishi wanapata mikataba na suala hili halina mjadala na tutalifanyia kazi'' amesema Waziri Bashungwa.
Sambamba na hilo Waziri Bashungwa, amesema wizara yake inaandaa utaratibu wa kuzungumza na wamiliki wa vyombo vya habari lengo ni kuweka ushirikiano katika kutimiza malengo ya serikali na kuboresha stahiki za wanahabari.
Chanzo - EATV
Social Plugin