Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : RPC MAGILIGIMBA AZINDUA MRADI WA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO....SPC, RAFIKI SDO, YWL, TAI NA HALMASHAURI YA SHINYANGA WAUNGANA.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba akionesha Mpango Mkakati wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto Mkoa wa Shinyanga wakati akizindua rasmi Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba amezindua rasmi Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga unaotekelezwa na Shirika la Rafiki SDO,Thubutu Africa Initiatives, Young Women Leadership, Shinyanga Press Club na halmashauri hiyo kwa ufadhili wa Shirika la Women Fund Tanzania (WFT). 

Uzinduzi huo umefanyika leo Januari 22,2021 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa mkoa, halmashauri, maafisa maendeleo ya jamii,maafisa watendaji wa kata, waandishi wa habari na wawakilishi wa mashirika yanayotetea haki za wanawake na watoto. 

Kamanda Magiligimba amesema suala la ulinzi wa mtoto ni la kila mtu katika jamii na kusisitiza kuwa ni wajibu wa kila kiongozi kuanzia ngazi ya mkoa,halmashauri,kata na kijiji kuhakikisha wanakuwa na mipango mikakati ya kuzuia unyanyasaji wa mwanamke na mtoto katika himaya zao. 

Aidha amempongeza Mkuu wa mkoa wa Shinyanga kwa kuweka Mpango Mkakati wa Mkoa katika kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia ifikapo mwaka 2025 ambao umekuwa chachu ya mabadiliko katika mkoa wa Shinyanga. 

“Nimtake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kutengeneza Sheria ndogo ambazo zitasaidia kila Mtendaji wa Kata au Kijiji kuhakikisha kwenye himaya yake hakuna mimba kwa wanafunzi wala ndoa za utotoni na kama zitatokea basi tujitahidi kumpata mtuhumiwa ili kupata hukumu ambayo itakuwa fundisho kwa jamii ili iachane na vitendo vya ukatili”,amesema Kamanda Magiligimba. 

Amelishukuru Shirika la Women Fund Tanzania kwa kufadhili mradi wa Ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambao utadumu kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Januari 2021 hadi Machi 2021. 

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba amesema mradi huo utakuwa chachu ya mabadiliko katika jamii ili kuondokana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. 

Hata hivyo amesema halmashauri hiyo inaendelea na utaratibu wa kuwa na Sheria ndogo katika kila kijiji ili kuchukua hatua dhidi ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika jamii. 

Kwa upande wake, Afisa Mradi wa Shirika la Women Fund Tanzania mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia amewasihi wadau waliopata ruzuku kutekeleza mradi huo ikiwemo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Rafiki Social Development Organization, Thubutu Africa Initiatives (TAI), Young Women Leadership ( YWL) na Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club –SPC) kuzingatia taratibu za utekelezaji miradi pamoja miongozo ya serikali. 

Amesema WFT inaendelea kupokea mawazo mazuri kutoka kwa wadau yatakayoleta matokeo chanya kwani shirika hilo lipo kwa ajili ya kuhudumia jamii na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na kufurahia nchi yao. 

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Alphonce Kasanyi amewataka watekelezaji wa mradi huo kutoa taarifa za fedha za mradi kwa wakati bila kuchelewa hata kidogo na kuepuka kutoa takwimu za uongo huku akiwasisitiza kufanya kazi kwa ushirikiano. 

Kwa upande wao, watekelezaji wa Mradi huo,wamesema wamejipanga kikamilifu katika kuhakikisha wanatekeleza mradi wa kutokomeza ukatili wa dhidi ya wanawake na watoto katika kata 13 ambazo ni Solwa, Lyabukande, Lyamidati, Nyamalogo, Mwalukwa, Pandagichiza, Ilola, Puni, Nyida, Usule, Mwamala, Itwangi na Masengwa. 

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lydia Kwesigabo aliwakumbusha watekelezaji wa mradi huo wasisahau kuyafikia makundi maalumu wakiwemo watu wenye ulemavu kwani wapo wanaofanyiwa matukio ya ukatili lakini hawapati nafasi ya kusemewa. 

Nao wadau walioshiriki uzinduzi huo wameshauri ushirikishwaji wa wazee maarufu, wa kimila wanaume wanaopendelea kwenye vijiwe vya kahawa, viongozi wa sungusungu,watoto,wasanii wa nyimbo za asili ‘marenga’ ili jamii ione kuwa huo ni mkakati halisi wa kuhamasisha kuachana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. 

Naye Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kutoka ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Analyse Kaika ameshauri jamii kutoa ushahidi kwenye kesi zinazohusu matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto huku Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto wilaya ya Shinyanga Victoria Maro akiwaomba wadau kulifikia pia kundi la wanawake wanaofanya biashara ya ngono na kuangalia vyanzo vya mimba kwa wanafunzi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba akizungumza leo Januari 22,2021 wakati akizindua rasmi Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga unaotekelezwa na Shirika la Rafiki SDO,Thubutu Africa Initiatives, Young Women Leadership, Shinyanga Press Club na halmashauri hiyo kwa ufadhili wa Shirika la Women Fund Tanzania (WFT). Kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba, Kushoto ni Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Alphonce Kasanyi. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba akizungumza leo Januari 22,2021 wakati akizindua rasmi Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga unaotekelezwa na Shirika la Rafiki SDO,Thubutu Africa Initiatives, Young Women Leadership, Shinyanga Press Club na halmashauri hiyo kwa ufadhili wa Shirika la Women Fund Tanzania (WFT). Wa kwanza kulia ni  Afisa Mradi Shirika la Women Fund Tanzania mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akifuatiwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba akizungumza leo Januari 22,2021 wakati akizindua rasmi Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba akizungumza leo Januari 22,2021 wakati akizindua rasmi Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga 
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Alphonce Kasanyi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga unaotekelezwa na halmashauri hiyo pamoja na Shirika la Rafiki SDO,Thubutu Africa Initiatives, Young Women Leadership, Shinyanga Press Club na halmashauri hiyo kwa ufadhili wa Shirika la Women Fund Tanzania (WFT).
Afisa Mradi wa Shirika la Women Fund Tanzania mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga unaotekelezwa na halmashauri hiyo pamoja na Shirika la Rafiki SDO,Thubutu Africa Initiatives, Young Women Leadership, Shinyanga Press Club na halmashauri hiyo kwa ufadhili wa Shirika la Women Fund Tanzania (WFT).
Afisa Mradi wa Shirika la Women Fund Tanzania mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga unaotekelezwa na halmashauri hiyo pamoja na Shirika la Rafiki SDO,Thubutu Africa Initiatives, Young Women Leadership, Shinyanga Press Club na halmashauri hiyo kwa ufadhili wa Shirika la Women Fund Tanzania (WFT).
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga unaotekelezwa na halmashauri hiyo pamoja na Shirika la Rafiki SDO,Thubutu Africa Initiatives, Young Women Leadership, Shinyanga Press Club na halmashauri hiyo kwa ufadhili wa Shirika la Women Fund Tanzania (WFT).
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga unaotekelezwa na halmashauri hiyo pamoja na Shirika la Rafiki SDO,Thubutu Africa Initiatives, Young Women Leadership, Shinyanga Press Club na halmashauri hiyo kwa ufadhili wa Shirika la Women Fund Tanzania (WFT).
Mratibu wa MTAKUWWA halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Aisha Omary akielezea kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga unaotekelezwa na halmashauri hiyo pamoja na Shirika la Rafiki SDO,Thubutu Africa Initiatives, Young Women Leadership, Shinyanga Press Club na halmashauri hiyo kwa ufadhili wa Shirika la Women Fund Tanzania (WFT).
Mratibu wa MTAKUWWA Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga , Aisha Omary akiwasilisha Mpango Kazi wa Halmashauri hiyo kuhusu namna watakavyotekeleza mradi wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini wakifuatilia uwasilishwaji wa mipango kazi ya utekelezaji wa mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Afisa Miradi wa shirika la Young Women Leadership (YWL), Veronica Massawe akiwasilisha mpango kazi namna watakavyotekeleza Mradi wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club -SPC), Estomine Henry akiwasilisha mpango kazi wa utekelezaji wa mradi wa Nafasi ya Vyombo vya Habari katika kumaliza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club -SPC), Estomine Henry akiwasilisha mpango kazi wa utekelezaji wa mradi wa Nafasi ya Vyombo vya Habari katika kumaliza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kutoka Shirika la Rafiki SDO, George Nyanda akiwasilisha mpango wa utekelezaji wa mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto walioupa jina la "Tuwalee".
Meneja Miradi kutoka Shirika la Thubutu Africa Initiatives ,Paschalia Mbugani akiwasilisha mpango kazi wao katika kutekeleza mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto  wilaya ya Shinyanga, Victoria Maro akichangia hoja wakati wa uzinduzi wa mradi wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Afisa Mradi wa Shirika la Women Fund Tanzania mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akichangia hoja wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga 
Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Salehe Hassan akichangia hoja wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kutoka ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Analyse Kaika akichangia hoja wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga 
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wilaya ya Shinyanga Faustine Sengerema akichangia hoja wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Mtoto Stephen Kiyenze akichangia hoja wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mtoto Irene Laurent akichangia hoja wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Meneja Miradi wa Shirika la ICS ,Sabrina Majikata akichangia hoja wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kuruthum Mlolwa kutoka shirika la PWWCO akichangia hoja ukumbini.
Mdau akichangia hoja ukumbini.
Mdau kutoka Shirika la TIDO akichangia hoja ukumbini
Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Agnes Ginethon akichangia hoja ukumbini.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Muhoja akizungumza ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba akipiga picha ya pamoja na wadau wa haki za wanawake na watoto baada ya kuzindua Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga unaotekelezwa na Shirika la Rafiki SDO,Thubutu Africa Initiatives, Young Women Leadership, Shinyanga Press Club na halmashauri hiyo kwa ufadhili wa Shirika la Women Fund Tanzania (WFT).

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com