Na Dotto Mwaibale - Dar es salaam
KANISA la Moravian Usharika wa Kijichi jijini Dar es Salaam limefanya bonanza la mpira wa miguu kwa ajili ya kusherehekea sikukuu za mwishoni mwa mwaka 2020.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi Mchungaji wa kanisa hilo Raphael Mwampagatwa alisema walifanya hivyo ili kuhubiri neno la Mungu kupitia michezo.
"Michezo mara zote ukusanya watu hivyo tuliona tufanye kitu kama bonanza ili tukikutana na watu mbalimbali tukumbushane neno la Mungu hasa katika sikukuu hizi na mwishoni mwa mwaka yaani chrismasi na mwaka mpya." alisema Mwampagatwa.
Mwampagatwa alisema mbali ya kuhubiri kupitia michezo pia uwajenga kiakili na kiafya na kufahamiana na watu wengine ambao wanaishi jirani na kanisa hilo.
Alisema muitikio wa watu kushiriki mchezo huo ulikuwa mkubwa hivyo mwaka huu Mungu akiwajaalia wataongeza michezo mingine mingi kama Netball, kukimbiza kuku, riadha, kukimbia huku ukiwa umevaa gunia miguuni, kuvuta kamba na uimbaji.
Social Plugin