JESHI la Polisi Mkoani Tanga limewakamata watu wanne wanaodaiwa kuwa ni Majambazi sugu waliokuwa wakitafutwa kwa muda
mrefu katika wilaya ya Korogwe akiwemo
kiongozi wa genge la uhalifu katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa
Tanga na nje ya mkoa na mlinzi wa kampuni ya Gomba Estate.
Watu hao wanaodaiwa kuwa ni Majambazi wamekamatwa mwishoni mwa wiki katika oparesheni ya Kikosi maalumu
cha jeshi la polisi iliyofanyika usiku wa kuamkia Januari 25 katika eneo
la kibaoni Mombo wilayani Korogwe .
Akizungumza leo na waandishi wa Habari Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda alisema watu hao wamekamatwa kutokana na Oparesheni ya iliyokuwa ikifanywa na kikosi maalumu
cha Jeshi hilo iliyofanyika usiku wa kuamkia Januari 25 katika eneo
la kibaoni Mombo wilayani Korogwe
aliwataja watu hao kuwa
ni pamoja na Hamis Mbelwa (46),Haji Semkondo,(42), wengine ni Barnaba
Simon (62)na Ally Babiwi wote ni wakazi wa Wilaya ya Korogwe.
Akifafanua
sifa za watu hao waliotafutwa kwa muda mrefu alisema majambazi wote wamekuwa wakifanya uhalifu wakutumia silaha,
"Kwa
mfano huyu Hamis Mbelwa alikuwa ni mfungwa katika gereza kuu la
mkoa wa Tanga Maweni na alihukumiwa miaka 30 jela mwaka 2015 katika
hukumu iliyotokana na kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha huko Korogwe
na alitoroka gerezani na kuungana na genge lake la uhalifu Juni 2019", Alisema Chatanda.
Aliongeza
kuwa kiongozi huyo wa genge baada ya kutoroka Gerezani mwezi Agosti
2019 aliongoza genge lake kufanya uporaji wa kutumia silaha hospitali ya
Rosmin iliyopo wilayani Korogwe na kufanikiwa kupora Shilingi milion
8.0.
Akizungumzia Barnaba Simon Maarufu kwa jina la Nyau spos, Chatanda alisema
amekuwa ni mlinzi kampuni ya Gomba Estate iliyopo wilayani Korogwe
lakini pia ni mshirika wa genge la uhalifu lililokuwa likiongozwa na Hamis
Mbelwa.
Alisema kwamba wamekuwa wakitumia silaha aina ya Shotgun yenye usajili
wa 328932 silaha ambayo hutumika kwenye matukio mbalimbali ya uhalifu,
"Huyu
ni mlinzi lakini pia ni mshirika wa genge la uhalifu la Hamis Mbelwa na
amekuwa akiwakodishia silaha majambazi wenzake kwa ajili ya utekelezwaji wa uhalifu",alisema Chatanda
Alisema wengine Haji Semkondo na Ally Juma ambao waliokuwa ni
washirika wa genge hilo nakwamba wamekuwa wakifanya uhalifu kwa kutumia
silaha hususani utekaji barabarani katika Barabara kuu ya Tanga
-Arusha na unyang'anyi wa kpikipiki .
Chatanda alisema msako wa kuwatafuta wahalifu wengine unaendelea ili kuwakamata wengine waliosalia na
watuhumiwa wengine ambao watakuwa wakijihusisha na uhalifu.
Social Plugin