Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU AWAJULIA HALI MAJERUHI WA AJALI YA TRENI DODOMA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Bi. Mariam Malembo (24) Mkazi wa Morogoro mmoja kati ya Majeruhi wa ajali ya Treni iliyotokea jana usiku katika eneo la Bahi Dodoma wakati Treni hiyo ikitokea Dar es salaam kuelekea Mkoani Kigoma, anayepatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Dodoma leo Januari 03,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan akiwajulia hali baadhi ya majeruhi
**
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewatembelea majeruhi na kuwafariji majeruhi wa ajali ya treni iliyotokea jana Januari 2, 2021 Dodoma wanaoendelea kupata matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma ambapo ametoa maagizo kwa mkoa kuhakikisha wanasaidiwa kufika makwao mara watakapopata nafuu.

Samia alitoa kauli hiyo baada ya kuzunguka katika wodi zote walikolazwa majeruhi hao na kuzungumza nao lakini akasema 

Kiongozi huyo amefika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma mapema saa moja asubuhi na mbali na kuzungumza na majeruhi wa treni lakini amezungumza na wagonjwa wengine akiwafariji.


Akiwa hospitalini hapo Mama Samia amesema ametembelea wodi zote na kuwaona majeruhi na kudai kuwa ameridhishwa na hali zao pamoja na huduma wanayopata wagonjwa hao.

Aidha ameeleza hatua ambazo zimechukuliwa mpaka sasa ikiwemo kuwasaidia usafiri wa kuendelea na safari abiria waliotoka salama pamoja na majeruhi wanaopona.

“Nawaagiza uongozi wa Mkoa, Wizara ya afya na Shirika la reli mshirikiane kuona wagonjwa hawa wanapata huduma zote na itakapothibitika wanaweza kuruhusiwa, wasaidieni wafike makwao salama,” amesema Samia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com