Kanda ya sauti imepatikana ambamo Rais Donald Trump wa Marekani anasikika akimshinikiza kamishna wa uchaguzi katika jimbo la Georgia kutafuta kura za kumsaidia Trump kushinda jimbo hilo katika uchaguzi wa rais wa Novemba iliyopita.
Katika kanda hiyo Trump anasikika katika mazungumzo ya simu na kamishna huyo, Brad Raffensperger akimtaka waziwazi kutafuta kura karibu 12,000 na kurudia mahesabu ya kura ili Trump atangazwe mshindi.
Kanda hiyo imewekwa hadharani na gazeti la Washington Post kuthibitisha hatua hiyo ya Rais Donald Trump, ambaye amepoteza kwa kura chache jimbo hilo la kusini mashariki mwa Marekani ambalo miaka ya nyuma lilikuwa ngome ya kutegemewa ya chama cha Republican chake rais Trump.
Makamu wa rais mteule, Kamala Harris amesema kitendo hicho cha Rais Trump ni matumizi mabaya ya madaraka.
Social Plugin