Mkutano wa "Tanzania Maternal Mortality and Nutrition - Mama Mjamzito na Mbogamboga" ambao umeandaliwa na Mbunge Neema Lugangira ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani ukiendelea
Mkutano wa "Tanzania Maternal Mortality and Nutrition - Mama Mjamzito na Mbogamboga" ambao umeandaliwa na Mbunge Neema Lugangira ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani ukiendelea
MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia NGOs Mhe Neema Lugangira ameandaa mkutano wa "Tanzania Maternal Mortality and Nutrition - Mama Mjamzito na Mbogamboga"
Mkutano huo ulilenga kujadiliana kuhusu
uhusiano kati ya vifo vya wakina mama wajawazito wanapojifungua na lishe
bora kwa maana ya upungufu wa damu "Anemia".
Katika mkutano huo zaidi ya watu 50 walishiriki kupitia Mtandao wa Zoom ambapo watoa mada waliwakilisha makundi muhimu .
Watoa
mada waliwakilisha makundi muhimu kama Dr. Grace Moshi - Msimamizi wa
Masuala ya Lishe; Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto na Dr. Lilian Mnabwiru - Katibu; Chama Cha Madaktari Tanzania
huku Anna Sengoka wa Chama Cha Wakunga Tanzania naye akiwasilisha mada.
Pia
katika mkutano huo uliwashirikisha Dr. Ali Said - Daktari Bingwa wa
Masuala ya Wanawake na Mwalimu MUHIMBILI na Dr. Isihaka Mwandalima -
Mkurugenzi (Technical) - Shirika lisilo la Kiserikali (NGO); Pathfinder
International
Mkutano
huu uliendeshwa na Wenyeviti Wawili Mhe Neema Lugangira (Mb.) na Dr.
Frank Minja; Rais wa Diaspora ya Watanzania wanaoishi Marekani.
Akizungumza
baada ya mkutano Mbunge Neema Lugangira alisema ni dhahiri mkutano huu
wa kwanza kwa hakika umedhihirisha umuhimu wa lishe bora kwa mama
mjamzito kabla, wakati na baada ya kujifungua.
Mhe
Mbunge alipoulizwa nini mchango wake katika kufanikisha suala hilo, alisema
kuwa Shirika la Agri Thamani Foundation ambalo yeye ni Mkurugenzi lipo
mstari wa mbele kuhamasisha ulaji wa matunda na mbogamboga ngazi ya kaya
hususan kwa vijana balehe.
Alieleza ndio maana shirika hilo limekuja na programu ya kutoa
msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike wa sekondari huku msaada
huu ukiendana na elimu ya lishe bora ikiwemo kuanzisha bustani za mfano
za mbogamboga shuleni na kaya.
Hata
hivyo Mhe Neema alisema ni dhamira yake kuendelea kuandaa mijadala ya
namna hii kwa njia mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha ajenda ya lishe
bora inapata kipaumbele inachostahili".