Mratibu wa Lishe kutoka Tamisemi Mwita Waibe akisistiza jambo wakati wa semina hiyo |
MSHIRIKI
kutoka wilaya ya Kyerwa akiomba Shirika la Agri Thamani liandae vitini
kwa ajili yao ili waingie field maana hawana muda wa kupoteza hii ni
ajenda kuu |
Viongozi wanawake wakifuatilia semina hiyo
MPANGO Jumuishi wa Lishe wa Taifa wa
Mwaka 2016-2021 unatambua Viongozi wa Kisiasa kama Wadau Muhimu katika
kuimarisha Lishe Bora na kutokomeza udumavu na aina zote za utapiamlo
nchini Tanzania.
Kulingana
na utambuzi huo, Agri Thamani imeendelea na mpango unaolenga kuwajengea uelewa
wa kina Viongozi wa Kisiasa ili waweze kutumia ushawishi wao kwenye
jamii kuchangia kubadilisha mfumo mzima wa mahusiano yetu na chakula na
pia waweze kufuatilia, kutathmini na kusimamia utekelezaji wa mipango
mizuri inayowekwa na Serikali.
Akizungumza
wakati wa semina ya kuwajengea uwezo viongozi wa UWT wilaya nne za Mkoa
wa Kagera ,Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Neema Lugangira (MB)
amesema katika jitihada za kuhakikisha kuwa mkoa huo unatokomeza
Udumavu maana
ndio Mkoa unaongoza kwa Idadi Kubwa Zaidi ya Watoto chini ya Umri wa
Miaka 5 wenye Udumavu;
Alisema
Shirika hilo lilianzisha Programu ya
kuwafikia Viongozi wa Jumuiya ya Umoja Wanawake Tanzania (CCM) ili
kuwajengea uwezo kwa lengo la kupata uelewa juu ya umuhimu wa lishe bora
na hatimaye kuweza kuwa chachu ya kutokomeza udumavu kwenye maeneo yao.
"Kama mnavyojua Makao
Makuu ya Agri Thamani yapo kwenye Majengo ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Kagera hivyo ni muhimu kwa Agri Thamani kuweka mikakati thabiti na
endelevu ili Mkoa wa Kagera uwe Mkoa wa Mfano katika Vita Dhidi ya
Udumavu na Utapiamlo kwa Ujumla", alisema Mhe Neema Lugangira (Mb) -
Mkurugenzi wa Agri Thamani.
Mkurugenzi huyo alisema katika kipindi cha mwezi Desemba 2020 hadi Januari 2021 Agri Thamani ilishatoa Semina
za Lishe Viongozi wa UWT kutoka Kata zote za Wilaya za Muleba, Bukoba
Mjini na Bukoba Vijijini. Pia, Agri Thamani imeshatoa Semina ya Lishe
kwa Madiwani wa Viti Maalumu kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Kagera.
Alisema kwa sasa Shirika hilo la Agri
Thamani limekamilisha Mafunzo ya Lishe kwa Awamu ya kwanza kwa
kuwafikia Viongozi wa UWT kutoka Kata zote za Wilaya za Ngara, Kyerwa,
Karagwe na Missenyi.
Mafunzo haya yalitolewa na Mbunge Neema Lugangira na Mratibu wa Lishe kutoka TAMISEMI, Ndg. Mwita Waibe.
Hata hivyo Viongozi hao wa UWT walionekana kushtushwa na hali ya lishe kwenye Mkoa na
maeneo yao kwa namna ambavyo watoto wanaweza kupata
athari pasipo mzazi kujua kumbe ambazo zinasababishwa na masuala ya
kilishe.
Kwa umoja wao waliazimia kuwa wanakwenda kuhoji kuhusu hali ya
lishe kwenye Kata zao, mikataba ya lishe iliyosainiwa kwenye kata zao,
bajeti za lishe zinazotengwa na Halmashauri zao na pia ajenda ya lishe
inakwenda kuwa ya kudumu kwenye shughuli zao.
Pia Waliaidi kuanza kutoa
mafunzo kwa jamii na wameiomba Agri Thamani iandae mafunzo ya vitendo
hususan kwenye eneo la namna bora ya kuandaa na kupika chakula chenye
lishe bora kwa mama mjamzito, mama anaenyonyesha na mtoto chini ya umri
wa miaka 5.
Katika
Awamu ya Pili ya Mafunzo haya, Agri Thamani inatarajia kuwafikia
Viongozi wa UWT na Madiwani kutoka Mikoa ya Kigoma, Tanga, Tabora, Lindi
na Geita kwa Wilaya zitakazochaguliwa. Aidha, chini ya Programu hii
hatua inayofuata ni kuwafikia Wenyeviti wa Serikali za
Mitaa/Vijiji/Vitongoji, Watendaji wa Kata, na Viongozi wengine Ngazi ya
Kata, Kijiji, Kitongoji na Jamii kwa jumla.
Mbunge
Neema Lugangira alimalizia kwa kusema wadau wote tukishikiriana kwa
karibu na kila mmoja kwa nafasi yake akaibeba Ajenda ya Lishe vita dhidi
ya kutokomeza udumavu na utapiamlo tutaishinda ndani ya miaka
mitano hii 2020-2025
Social Plugin