Na Fredy Mgunda na Denis Mlowe ,Iringa.
TIMU
ya soka ya Mtwivila city (Ifuenga united) imefanikiwa kuingia fainali
ya ligi soka daraja la tatu mkoa wa Iringa kwa baada ya kuifunga timu ya
soka Irole fc mabao 2 - 1 katika mchezo mkali wa nusu fainali ya pili
iliyochezwa kwenye uwanja wa Mkwawa.
Hivyo
kutokana matokeo hayo timu ya soka ya Ifuenga United watakutana na
Ivambinungu fc siku ya jumapili katika mchezo utakaopigwa uwanja wa
Samora.
Timu ya
Ivambinungu Fc ilikuwa timu ya kwanza kutangulia kwenda fainali baada ya
kuwafunga timu ya Kidamali Fc kwa jumla ya magoli 3-1 na kuifanya timu
hiyo kufika fainali baada ya kushinda nusu fainali zote mbili
zilizopigwa katika viwanja vyote viwili vya nyumbani na ugenini.
Nayo
Timu ya Mtwivila city (Ifuenga united) imeingia fainali baada ya
kuifunga timu ngumu ya Irole Fc kwa jumla ya goli mbili moja baada ya
michezo yote miwili iliyochezwa nyumbani na ugenini.
Akizungunza
mara baada ya mchezo wa nusu fainali ya pili kocha wa timu ya Ifuenga
Edger Nzelu alisema kuwa timu hiyo imejipanga vilivyo kuhakikisha
wanashinda fainali kwa kuwa mchezo huo muhimu ambao kwa namna yoyote ile
lazima washinde kwenda katika ngazi ya kanda.
Nzelu
alisema kuwa baada ya kushinda mchezo huo mgumu wa nusu fainali ana
uhakika wa kushinda mchezo wa fainali yenyewe kwa kuwa timu hiyo ya
Irole Fc ndio ilikuwa kikwazo kwao.
Aliwataka
mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuisapoti timu hiyo ili kuipa nguvu
kuhakikisha kwenye fainali na kwenda mbele kwenye mashindano ngazi
nyingine
Naye mfadhili wa
timu hiyo Joseph Kilienyi alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha
wanashinda mchezo wa fainali na kuchukua kombe hilo.
Alisema
kuwa timu ya Ivambinungu Fc ni timu nzuri lakini wao wamejipanga
kuhakikisha wanashinda mchezo huo muhimu kwao kwa kuwa wanataka kwenda
kanda na kuhakikisha timu hiyo inafika katika madaraja ya juu na
hatimaye kufika ligi kuu Tanzania Nara.
Timu
ya Mtwivila city (Ifuenga) imejipanga kwa kila kitu hivyo wakiwa
mabingwa wa mkoa watahakikisha timu hiyo hairudi nyuma tena kwenye ligi
ya mkoa wa Iringa tena.
Bingwa
wa ligi hiyo iliyojizoelea umaarufu nchini kutokana na udhamini wa
kampuni ya maziwa ya Asas ataondoka na sh milioni 2.5 huku mshindi wa
pili akichukua milioni 1.5 na mshindi wa tatu ataibuka na laki 750000
baada ya zawadi kuongezwa kwa washindi.