Mtu aliyetambuliwa kwa jina la Juma Kitemango (48) mkazi wa Matundasi Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya, ameuawa kwa kushambulia na vitu vyenye ncha kali na mgoni wake, Juma Sunzima (40) baada ya kuwafumania na mkewe wakiwa ndani ya chumba chake.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Jerome Ngowi, amewaambia waandishi wa habari Januari 6 jijini humo kuwa tukio hilo lilitokea Januari 4 wilayani humo, baada ya marehemu kufika nyumbani kwake na kumkuta mkewe Merry Daimon, akiwa na mwanaume aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wake.
"Marehemu aliwafumania mkewe na mtuhumiwa wakiwa wanafanya yao ndani ya nyumba yake waliyokuwa wakiishi na mkewe na ndipo ulipotokea mzozo na mtuhumiwa kumjeruhi na vitu vyenye ncha kali na sehemu za kichwani na utosini na kusababisha kifo chake," alisema.
Asema mara baada ya tukio hilo mke wa marehemu na mtuhumiwa walikimbia na kwamba jeshi la polisi linaendelea na msako ili wafikishwe mikononi mwa sheria.
Alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mareheme kabla ya umauti kumkuta walikuwa na migogoro isiyokwisha na mkewe ya kimahusiano iliyohusihwa na wivu wa kimapenzi.
Social Plugin