Hatimaye wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika Simba SC wamepangwa kundi A sambamba na mabingwa wa watetezi Al Ahly, Namungo nayo imepangwa kucheza na Primeiro De Agosto kwenye kombe la shirikisho hatua ya mtoano, kwenye droo iliyofanyika hii leo Cairo Misri.
Simba wamepangwa Kundi moja na Al Ahly , Al Merreik na AS Vita
Shirikisho la soka barani Afrika Caf, Alasiri ya leo imeendesha droo ya wazi ya upangaji makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika pamoja na kupanga timu zitakazokutana kwenye hatua ya mtoano kuwania kufuzu hatua ya makundi kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika.
Wekundu wa msimbazi Simba ambaye ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika imepangwa kundi A na Al Ahly ya Misri, Al Merreik ya Sudan na AS Vita kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na michezo hiyo ikitazamiwa kuanza 14 Februari 2021.
Hii ni mara ya pili Simba kupangwa na Al Ahly ambayo ni bingwa wa kihistoria wa michuano hiyo pamoja na klabu ya AS Vita ya DR Congo baada ya kupangwa nao kundi moja msimu wa mwaka 2018-19 msimu ambao Simba alifanikiwa kuishia hatua ya robo fainali ya klabu bingwa Afrika.
Simba walikata tiketi ya kucheza hatua ya makundi baada ya kuiondoa Plateua United ya Nigeria kwenye mchezo wa hatua ya awali kwa ushindi wa jumla wa bao 1-0, kwenye hatua iliyopita ambayo ni raoundi ya kwanza wakaitupa nje ya mashindano FC Platnum ya Zimbabwe kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1 kwenye michezo ya mikondo miwili.
Klabu ya Namungo ambayo ndiyo wawakilishi wa Tanznaia kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ikiwa inacheza mashindano haya kwa mara a kwanza imepangwa kucheza dhidi ya klabu ya Primeiro de Agosto ya Angola kwenye michezo miwili ya mtoano kuwania kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika, mchezo wa kawanza utachezwa kuanzia tarehe 14 februari 2021 na marudiano kupigwa tarehe 21 februari 2021.
Social Plugin