UBORA WA VIWANDA VYA NYAMA NCHINI WACHANGIA KASI YA USAFIRISHAJI NYAMA NJE YA NCHI

 

Kasi ya kusafirisha nyama kwenda nje ya nchi imeongezeka kutokana na kuwepo kwa ubora wa Viwanda vya nyama ikiwa ni uwekezaji mkubwa uliopo jambo linalosababisha kuwepo kwa nyama bora na salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu na kukidhi soko la ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania Bwana Imani Sichalwe akiwa kwenye ziara ya kukagua mazingira ya usafirishaji wa nyama kutoka Tanzania kwenda nchi za nje aliyoifanya tarehe 16.01.2021 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere Jijini Dar.

Uwepo wa viwanda hivi vya nyama vya kisasa hapa Nchini ndio vinafanya tuwe na ithibati ya kupeleka nyama nje ya nchi ambapo kiwanda Cha Tanchoice kilichopo Kijiji cha soga wilayani Kibaha Mkoani Pwani chenye uwezo wa kuchinja mbuzi 4500 kwa siku na ng’ombe 1000 kwa siku moja ambapo kwa Tarehe 16.01.2021 kimepeleka mbuzi 2000 waliochinjwa Sawa na kilo 20,000 au tani 20 kwenda Oman na Kuwait.

“Kwa Sasa kwa wiki kiwanda cha nyama cha Tanchoice kilichopo Kibaha Mkoani Pwani husafirishwa mbuzi waliochinjwa 6000 sawa na kilo 60,000 sawa na tani 60 kwenda Omani,Qatar na Kuwait na kwa wiki ijayo kiwanda kitaanza kupeleka nyama katika soko jipya la Hongkong. Kwa upande wa kiwanda Cha Nyama Cha Eliya Foods Overseas Limited kimeanza kupeleka nyama kwenda Oman Mbuzi 1874 sawa na tani 14.6” amesema Sichalwe.

Katika ziara hiyo ya kukagua mazingira ya usafirishaji wa nyama kwenda nje ya nchi Kaimu msajili Bodi ya Tanzania amesema ameridhika na namna shughuli nzima ya utaratibu unaofanywa kuanzia kushusha nyama kwenye gari,kuingiza kwenye vyumba maalumu vya kuhifadhia nakupooza pamoja na namna ya upakiaji wa nyama hizo kwenye ndege.

 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post