Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UINGEREZA YAPIGA MARUFUKU ABIRIA KUTOKA TANZANIA, DRC


Serikali ya Uingereza imepiga marufuku abiria kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuzuia maambukizi ya aina mpya ya virusi vya corona.

"Ili kusaidia kuzuia kuenea kwa aina ya COVID-19 iliyogundulika Afrika Kusini, tunapiga marufuku abiria wote wanaoingia kutoka Tanzania na DRC kuanzia saa 10 alfajiri kesho (Ijumaa)," ameandika Bw Grant Shapps, waziri wa usafirishaji nchini Uingereza kupitia mtandao wake wa Twitter Alhamisi usiku.

"To help to stop the spread of the COVID-19 variant identified in South Africa, we are banning all arrivals from Tanzania and Democratic Republic of Congo from 4am tomorrow.— Rt Hon Grant Shapps MP (@grantshapps) January 21, 2021"

Zuio hilo linaanza kwa wasafiri wote waliotoka ama kupita nchini Tanzania na DRC ndani ya siku 10 zilizopita. Hata hivyo, raia wa Uingereza na Ireland na raia kutoka mataifa mengine ambao wenye vibali vya ukaazi wataruhusiwa kuingia ila watatakiwa kujitenga nyumbani pamoja na familia zao kwa siku 10 baada ya kuwasili.

Tanzana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimeongezwa kwenye orodha ya Uingereza ya nchi zilizopigiwa marufuku ya wasafiri wake kuingia nchini humo kama hatua yza kudhibiti maambukizo ya aina mpya ya virusi vya Corona vilivyogunduliwa nchini Afrika kusini.

Awali mwezi huu mataifa mengine 11 ya Afrika yalipigwa marufuku kama hiyo. Mataifa hayo ni; Namibia, Zimbabwe, Botswana, Eswatini, Zambia, Malawi, Lesotho, Msumbiji na Angola - visiwa vya Ushelisheli na Mauritius.

Uingereza ilipiga marufuku abiria kutoka Afrika Kusini Desemba 24.

Uingereza ni miongoni mwa mataifa ambayo yanakabiliana na janga la virusi vya corona kwa kiwango kikubwa na uchumi wake ukiwa umeyumba kutokana na wimbi la kwanza la virusi mambukizi ya corona.

CHANZO- BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com