VYUO VIKUU NCHINI VYAASWA KUTOA WATAALAMU WENYE UJUZI WA KUJIAJIRI

Katibu Mkuu wa Elimu,Sayansi Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo akizungumza katika kikao cha wadau kujadili rasimu ya miongozo ya usalama wa mazingira na jamii katika utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya juu wa mabadiliko ya kiuchumi (HEET) nchini kilichofanyika leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Katibu Mkuu wa Elimu,Sayansi Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo akizungumza katika kikao cha wadau kujadili rasimu ya miongozo ya usalama wa mazingira na jamii katika utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya juu wa mabadiliko ya kiuchumi (HEET) nchini kilichofanyika leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Wadau mbalimbali wakifuatilia kikao cha wadau kujadili rasimu ya miongozo ya usalama wa mazingira na jamii katika utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya juu wa mabadiliko ya kiuchumi (HEET) nchini kilichofanyika leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Vyuo Vikuu nchini vimeaswa kutoa wataalamu wenye ujuzi wa kuweza kujiajiri na kuajirika ikawa lengo ni kuwa na mitaala yenye kulenga soko nyumbulifu kwa kadri ya mabadiliko ya teknolojia.

Ameyasema hayo leo Katibu Mkuu wa Elimu,Sayansi Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo katika kikao cha wadau kujadili rasimu ya miongozo ya usalama wa mazingira na jamii katika utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya juu wa mabadiliko ya kiuchumi (HEET) nchini kilichofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho Dkt.Akwilapo amesema kunatakiwa kufanyike maboresho makubwa ya mfumo wa utoaji wa elimu ya juu ambayo yatasababisha kuwe na mabadiliko chanya kwenye nyanja zote zinazohusiana na ukuzaji wa uchumi wa nchi yetu.

"Uwepo wa mradi huo utaleta madiliko na mapinduzi katika kujenga uchumi wa kisasa hapa nchini Tanzania". Amesema Dkt.Akwilapo.

Aidha amesema kuwa Serikali ina lengo la kukopa fedha kutoka Benki ya Dunia ili kutekeleza mradi wa kuboresha elimu ya juu kwa ajili ya kuimarisha uchumi nchini.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Wanafunzi Wenye mahitaji Maalumu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Bw.Kelvin Mkude amesema mradi wa HEET umekuja katika wakati muafaka kwani umelenga kwa wale wahitimu wa Vyuo Vikuu wawe vizuri katika upande wa ajira hasa kujiajiri.

Naye mwakilishi wa Taasisi ya Serikali ya wanafunzi DARUSO Bi.Ntoteba Hassani amesema mradi huo utawasaidia wanafunzi ambao wapo Vyuo Vikuu kuboresha zaidi mnyororo mzima wa elimu ya Vyuo Vikuu lkiwemo miundombinu kwa kuwezesha watu kupata ajira na kuweza kujiajiri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post