Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akizungumza wakati
wakati wa hafla ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa kutoka shirika la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji maziwa Tanzania (TMPP) iliyofanyika katika kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga kushoto aliyekaa ni Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB Jeremiah Mhada
Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxoakizungumza wakati wa halfa hiyo
Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB Jeremiah Mhada akieleza jambo wakati wa halfa hiyo
Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamunguakizungumza wakati wa halfa hiyo
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kushoto akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa kutoka shirika la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji maziwa Tanzania (TMPP) iliyofanyika katika kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga kulia ni Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxo
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kushoto akimshukuru Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxo mara baada ya makabidhiano hayo kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga katika halfa hiyo
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akiwasha moja ya magari hayo
WAFUGAJI nchini wametakiwa kubadilika na kuachana na
ufugaji wa mazoea bali wafuge kisasa kwa ajili ya kupata mazao mengi
lakini yenye ubora ambayo yataweza kuuzika kwa faida na hivyo kuongeza
mchango wa pato la Taifa.
Ushauri
huo umetolewa na Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba
Ndaki wakati wa hafla ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa kutoka
shirika la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji maziwa
Tanzania (TMPP) iliyofanyika katika kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo
Jijini Tanga.
Alisema
kuwa licha ya Tanzania kuwa na mifugo mingi lakini sekta hiyo mchango
wake kwenye pato la taifa ni asilimia 7.9% pekee kutokana na ufugaji wa
kimazoea ambao hautoi matokeo bora.
Akizungumzia
uzalishaji wa maziwa nchini Waziri Ndaki alisema ni lita Bil 3.01 huku
kati ya hizo lita Mil 2.1 zinatokana na ng'ombe wa asili Mil 31 huku
ng'ombe wa kisasa Mil 2 wanatoa lita bil 0.9.
"Kutokana
na uzalishaji mdogo wa maziwa hata kiwango cha unywaji wa maziwa kwa
mwananchi mmoja mmoja kimekuwa kidogo kwani kwa mujibu wa takwimu ni
lita 54 kwa mwaka sawa na kijiko kimoja kwa siku" alisema Waziri Ndaki.
Nae
Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamungu alisema kuwa uwepo wa mradi
umesaidia kuongeza kasi ys uanzishwaji wa viwanda vya maziwa hadi
kufikia vitano ambavyo vinazalisha maziwa kwa kutumia teknolojia ya UHT.
Alisema
kuwa bado kumekuwepo na changamoto katika eneo la ukusanyaji wa maziwa
kwani kuna kiasi kikubwa yanakuwa hana kosa ubora kabla ya kufika soko
hivyo kuwa hasara kwa mfugaji.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji na masoko kutoka
wizara ya mifugo na uvuvi Steven Maiko alisema kuwa kutokana na
tathimini waliyoifanya 2016/17 inaonyesha kuwa ifikapo mwala 2030/31
sekts hiyo itakabiliwa na upungufu mkubwa raslimali zake za nyama na
maziwa kutokana na ongezeko la idadi ya watu.
Hivyo
kutokana na changamoto hiyo serikali kwa kushirikiana na wahisani
waliamua kuja na mradi huo ili kuongezs uzalishaji, kudhibiti magonjwa
ya mifugo lakini.na kuongeza mnyororo wa thamani wa maziwa ikiwemo kuweka mazingira safi ya kufanyabiashara.
Nae
Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la
Helfer Mark Tsoxo alisema kuwa lengo la mradi wa TMPP kuongeza kipato
kwa wafugaji wapatao 50, 000 nchi nzima na kwa kipindi cha miezi mitatu
pekee tayari wameweza kuwafikia wafugaji 45, 000 kwa kuwapa mafunzo ya
ufugaji wa kisasa ili waweze kupata mazao bora na ambayo yataweza kuuza
kwa urahisi.
Alisema kwa
upande wa wasindikaji waweze kuwawezesha vifaa ili kuhakikisha
wanaboresha ukusanyaji wa maziwa na kudhibiti ubotevu wake ili
kumuhakikishia mfugaji soko lenye uhakika.
Nae
Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB Jeremiah
Mhada alisema kuwa benki hiyo imewawezesha wafugaji mkopo wa zaidi ya
sh Mil 396 pamoja na mitamba bora.
"Ili
kuongeza kipato kwa wafugaji wadogo tumewawezesha kupata mitamba ya
kisasa na kiwaunganisha ns masoko ili kuongeza thamani na kuchoches
kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini" alisema Mhada.
Social Plugin