Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk. Leonard Chamuriho akitoa hotuba kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Uchukuzi katika ukumbi wa Chuo Cha Benki Kuu Mwanza Januari11, 2021.
Kaimu Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi Gabriel Migire akizungumza kwenye Mkutano huo
Wajumbe wa Baraza wakiwa ukumbini
Wajumbe wa Baraza wakiwa ukumbini
Wajumbe wa Baraza wakiwa ukumbini.
Na Hellen Mtereko Mwanza
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ,Dkt. Leonard Chamuriho amewataka wafanyakazi wa sekta ya Uchukuzi kujenga tabia ya kujiendeleza kielimu ili wafanye kazi kwa weledi.
Ameyasema hayo leo Januari 11,2021 wakati akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa sekta hiyo Jijini Mwanza wenye lengo la kujadili utekelezaji wa majukumu ya kazi, utawala na wajibu wa wafanyakazi.
Alisema kila mtumishi ana wajibu wa kufanya kazi kwa weledi na ushirikiano ili kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu ya sekta hiyo.
Alisema hatutasita kuchukua hatua pale tutakapobaini mazoea yanawekwa mbele badala ya weledi katika utendaji wa kazi.
Aliongeza kuwa ni lazima wajibu uambatane na uelewa wa majukumu ya kila mmoja pamoja na uhusiano mwema kazini Kati ya viongozi na wafanyakazi.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa sekta hiyo Gabriel Migire alisema katika mpango wa tatu wa maendeleo ya Taifa unaoendelea kuandaliwa sekita hiyo imepewa dhamana ya kutekeleza miradi ya kielelezo ikiwemo ujenzi wa reli ya Kati, uboreshwaji wa Bandari ya Dar -es Salaam na uimarishaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania
Alisema utekelezaji wa miradi hiyo unasimamiwa na wajumbe wa sekta hiyo hivyo amewaasa kutekeleza miradi hiyo kwa ubora unaotakiwa na kulinda thamani ya fedha iliyowekezwa.
Naye Mjumbe kutoka Sekta ya Uchukuzi Stella Katondo alisema atahakikisha wanafanya kazi kwa weledi na bidii ili waweze kukamilisha miradi iliyopo kwenye sekta hiyo.