Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba
**
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshilikilia sungusungu wa kijiji cha Nyamalogo Fedson Matekele na William Desdez (27) muuguzi wa zahanati ya Nyamalogo kwa kosa la wizi wa dawa za binadamu katika zahanati hiyo iliyopo katika kata ya Nyamalogo wilaya ya Shinyanga na kuziuza nyumbani.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba tukio hilo limetokea Januari 12,2021 majira ya saa tisa kamili alasiri katika kijiji cha Nyamalogo, kata ya Nyamalogo, tarafa ya Nindo, halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kamanda Magiligimba amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa dawa hizo zabinadamu ziliibiwa zahanati ya Nyamalogo na kwamba baadhi ya dawa hizo zimekwisha muda wake wa matumizi 'Zime - expire' lakini zimekuwa zikiuzwa na mtuhumiwa Fedson Matekele.
Akifafanua zaidi kuhusu tukio, Kamanda Magiligimba amesema siku ya tukio uongozi wa kijiji cha Mwang'osha ulipokea taarifa kwamba kuna dawa za binadamu mali ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinauzwa nyumbani kwa mtuhumiwa Fedson Matekele ambaye ni sungusungu wa kijiji cha Nyamalogo.
“Kufuatia tukio hilo jeshi la polisi mkoani Shinyanga kwa kushirikiana na Kaimu Afisa Mtendaji wa kijiji cha mwang'osha tulifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wawili pamoja dawa hizo mbalimbali za binadamu ambazo ni Depoprovera -Zivals ,Mrdt-23-strip,Ors-2 satchets, Female condoms o3pcs, Benexylpenillis injection 2 vial , Furasemicle injection 4 amps, Butter sd , Bioline 4 bottle ,baadhi ya dawa hizo zimekwisha muda wake wa matumizi lakini zimekuwa zikiuzwa na mtuhumiwa Fedson”,ameeleza Kamanda Magiligimba.
“Watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya kukamilisha uchunguzi.Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga waendelee kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za uharifu na wahalifu”,ameongeza.
Social Plugin