Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Breaking : RAIS MAGUFULI AMTEUA DKT. BASHIRU ALLY KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI...ANACHUKUA NAFASI YA BALOZI KIJAZI


Dkt. Bashiru Ally Kakurwa

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. John Magufuli na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ally ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi (Picha kutoka Maktaba) 

                                                          ***
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi kuchukua nafasi ya Balozi Mhandisi John Kijazi aliyefariki dunia Februari 17,2021.

Wakati huo huo Rais Magufuli amemteua Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Balozi na kwamba uteuzi huo unaanza rasmi leo Ijumaa Februari 26,2021 na ataapishwa kesho saa tatu asubuhi Ikulu jijini Dar es salaam

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com