Picha : BENKI YA CRDB SHINYANGA YAZINDUA RASMI HUDUMA YA 'BENKI NI SIMBANKING' MZIGO UMEBORESHWA...MALUNDE ALAMBA UBALOZI

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga imezindua rasmi Huduma za fedha kupitia Simu ya mkononi 'Sim Banking' iliyoboreshwa kupewa jina la Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ itakayowawezesha wateja kufanya huduma zote za kibenki kupitia simu zao popote walipo. 

Uzinduzi huo umefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga ukiongozwa na Meneja wa Benki hiyo, Luther Mneney na kuhudhuriwa na wateja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mneney amesema Huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’  itafanyika katika matawi yote na itawawezesha wateja kupata huduma nyingi zaidi za kibenki kupitia simu ya mkononi na kwa urahisi zaidi ili kufurahia benki ya CRDB.

“Ukiwa ni simu basi una huduma zote za kibenki kidigitali zaidi. Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ inachukua nafasi ya huduma yetu ya mwanzo ya Simbanking lakini hii ni babu kubwa, tumeiboresha sana ili kuwafanya wateja wafurahie huduma zetu”,amesema Mneney.

“Wanachotakiwa kufanya wateja wetu kupiga *150*03# au kupakua CRDB SimBanking Playstore au Appstore na kupata huduma za kibenki zilizoboreshwa zaidi”,amesema Mneney.

Akielezea kuhusu Benki ni SimBanking ‘ Mzigo Umeboreshwa’, Afisa wa Benki ya CRDB, Lewis Temu amesema kupitia huduma hiyo yenye mpangilio mzuri, wateja wataweza pia kupata huduma za bima kiganjani ambapo TIRA imeunganishwa.

“Mteja atafungua akaunti kwa kutumia namba ya NIDA, kuhamisha fedha kirahisi,kutoa fedha kwenye ATM,matawi na mawakala,uwezo wa kurekodi miamala yote,kupata taarifa,kupata token ya umem papo hapo,kufunga na kufungua kadi,kuomba kadi,kulipia luku. DSTV na huduma zingine kabambe ikiwa ni pamoja na kutoa fedha hadi shilingi milioni 8”,amesema Temu.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui amesema wameamua kuboresha huduma za  kibenki mara kwa mara kutokana na mahitaji makubwa ya wateja kiuchumi ndiyo wameamua kuja na mzigo mpya ulioboreshwa na kuwaomba wateja waliohudhuria uzinduzi huo kuwa mabalozi wazuri.

Naye Meneja Biashara wa CRDB Kanda ya Magharibi,Jumanne Wagana alimtangaza Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde kuwa Balozi wa Benki ni SimBanking ‘ Mzigo Umeboreshwa’ Kanda ya Magharibi akisema Malunde 1 blog ni mtandao wa kijamii unaofanya vizuri nchini Tanzania.

Akizungumza kwa niaba ya wateja waliohudhuria uzinduzi huo, Barikiel Somboi ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuendelea kufanya ubunifu mara kwa mara ili kukidhi mahitaji ya wateja.

 ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney akizungumza leo Alhamis Februari 25,2021 wakati wa uzinduzi wa huduma ya fedha kupitia simu 'Sim Banking' iliyoboreshwa kupewa jina la Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ itakayowawezesha wateja kufanya huduma zote za kibenki kupitia simu.  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney akizungumza leo Alhamis Februari 25,2021 wakati wa uzinduzi wa huduma ya fedha kupitia simu 'Sim Banking' iliyoboreshwa kupewa jina la Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ itakayowawezesha wateja kufanya huduma zote za kibenki kupitia simu. 
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney akizungumza leo Alhamis Februari 25,2021 wakati wa uzinduzi wa huduma ya fedha kupitia simu 'Sim Banking' iliyoboreshwa kupewa jina la Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ itakayowawezesha wateja kufanya huduma zote za kibenki kupitia simu. 
Afisa wa Benki ya CRDB, Lewis Temu akielezea kuhusu Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’.
Afisa wa Benki ya CRDB, Lewis Temu akielezea kuhusu Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’.
Keki na vinywaji mbalimbali wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ' Mzigo Umeboreshwa' katika benki ya CRDB Tawi la Shinyanga.
Meneja Biashara Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamis Iddi akifungua Keki maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Keki maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja Biashara Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamis Iddi akizungumza wakati wa zoezi la kukata keki maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Mteja wa Benki ya CRDB Joab Kaijage akikata Keki maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Mteja wa Benki ya CRDB Joab Kaijage akikata Keki maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Mteja wa Benki ya CRDB Joab Kaijage akikata Keki maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) akimlisha keki mteja wa Benki ya CRDB Joab Kaijage wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Mteja wa Benki ya CRDB Joab Kaijage (kushoto) akimlisha keki Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Mteja wa Benki ya CRDB Joab Kaijage (kulia) akimlisha keki Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) akimlisha keki mteja wa Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) akimlisha keki mteja wa Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) akijiandaa kugawa keki kwa wateja na wafanyakazi wa benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Mteja wa Benki ya CRDB, Barikiel Somboi akiipongeza benki hiyo kwa kuendelea kuboresha huduma za kibenki akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa  ndani ya benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (kushoto) akimkabidhi Note Book ya Benki ya CRDB, Mkurugenzi wa Mtandao wa Habari wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde baada ya kumtangaza kuwa Balozi wa 'Benki ni SimBanking' Kanda ya Magharibi wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui (kushoto), Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana na Meneja  Biashara Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi wakigonga Cheers  wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Afisa Biashara Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akimhudumia vitafunwa mteja wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akigonga cheers na wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akigonga cheers na wafanyakazi wa benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa ndani ya benki wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Picha ya pamoja wateja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post