Na Peter Saramba - Mwananchi
Mtoto mwenye umri wa miaka minane (jina linahifadhiwa) mkazi wa mtaa wa Mission jijini Mwanza anaugulia majeraha kwenye makalio baada ya kuchapwa kwa waya huku akiwa amepakwa chumvi kwa tuhuma za kuiba Shilingi 1200.
Ukatili dhidi ya mtoto huyo anayesoma darasa la pili katika shule ya msingi Sahara jijini Mwanza unadaiwa kutendwa na baba yake mzazi Februari Mosi, 2021.
Mwalimu wa darasa ndiye aliyebaini majeraha ya mtoto huyo kwenye makalio yote mawili baada ya kumtilia shaka kutokana na kuchechemea kila alipotembea.
Akizungumza akiwa chini ya ulinzi, mama wa kambo wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Auliditensia Bwire amesema siku ya tukio, mume wake aliyemtaja kwa jina la Rahman Suleiman alimtuhumu mtoto wake kuiba Sh1, 200 ndipo alipoanza kumchapa huku akimpaka chumvi kwenye makalio.
Via Mwananchi
Social Plugin