Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAFURIKO YA DAMU YAZUA GUMZO KIJIJINI


Msichana mdogo akitembea katika mafuriko hayo mekundu katika eneo la Pekalongan, katikati ya mkoa wa Java Indonesia
***
Kijiji kimoja cha Indonesia kimekumbwa na mafuriko yenye rangi ya damu baada ya maji kuingia katika kiwanda kimoja cha nguo.

Rangi iliYokuwa ikitumika katika nguo ilisombwa na maji hayo na kusafirishwa katika barabara za kijiji cha Jenngot katikati ya eneo la Java siku ya Jumamosi.

Eneo hilo lililopo kusini mwa mji wa Pekalongan linasifika kwa tamaduni yake ya viwanda vya kutia nguo rangi.

Maelefu ya watu mitandaoni waliasambaza picha za maji hayo yenye rangi katika kijiji hicho.

Afisa mmoja wa shirika la misaada alithibitisha kuwa picha hizo zilikuwa za kweli.

''Mafuriko hayo ya rangi ya damu yanatokana na rangi za kuweka katika nguo ambazo zilisombwa na mafuriko'', Dimas Arga Yudha aliambia chombo cha habari cha Reauters.

''Itapotea baada ya kuchanganyika na maji ya mvua baada ya muda''.
Watu wakipeleka pikipiki katika maji ya mafuriko mekundu yanayotokana na rangi za nguo katika viwanda vya eneo la Pekalongan, Indonesia
*
Mito katika eneo la Pekalong imebadilisha rangi kutokana na rangi hiyo ya nguo huku mafuriko ya rangi ya kijani yakikumba kijiji kingine mwezi uliopita , kulingana na Reuters.

Indonesia mara kwa mara hukumbwa na mafuriko huku takriban watu 43 wakifariki kutokana na kimbunga kilichopiga mji mkuu Jakarta mapema mwaka huu.

Wakaazi walitumia ndege kumwagia kemikali mawingu ili kuzuia mvua huku mafuriko mabaya yakiripotiwa katika eneo hilo tangu 2013.
Wakaazi wakitembea katika mafuriko hayo ya rangi ya damu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com