Muonekano wa gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ yenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga likiwa nje ya Ofisi za CWT mkoa wa Shinyanga baada ya kuletwa na Kampuni ya Uagizaji Magari ya Dellah Car Traders Company leo Ijumaa Februari 5,2021.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kampuni ya
Uagizaji wa Magari nje ya nchi maarufu Dellah
Car Traders Company imekabidhi rasmi gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za
usajili T 682 DVJ yenye thamani ya shilingi milioni 49.9 ililoagiza kwa ajili
ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga.
Kampuni hiyo
ya Uagizaji wa Magari nje ya nchi Dellah
Car Traders Company yenye makao makuu Mjini Shinyanga na tawi la Dar es salaam
Magomeni Usalama Jengo la 3D imekabidhi gari hilo ililoliagiza Japan leo Ijumaa
Februari 5,2021 kwa Mwenyekiti wa CWT mkoa wa Shinyanga, John Balele
Shangwe za walimu
kupokea gari hilo zilianzia katika ofisi za Dellah Car Traders Company ambapo
wamefanya maandamano wakipita katika mitaa mbalimbali mjini Shinyanga kuelekea
katika ofisi cha Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) mkoa wa Shinyanga ambapo hafla
fupi ya makabidhiano ya gari imefanyika.
Akizungumza
wakati wa Kukabidhi gari hilo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders
Company inayojihusisha na uagizaji magari Japan, Dubai, Singapore na UK, Edwin
Charles Dellah amesema waliagiza gari hilo Japan Desemba 16,2020 na gari hiyo
imefika ndani ya siku 45 ambapo imefika Dar es salaam Januari 28, 2021 na wamekabidhi leo
Februari 5,2021.
Mkurugenzi
huyo amekishukuru Chama Cha Walimu Manispaa ya Shinyanga kuiamini Kampuni hiyo
mama kuagiza gari hilo ambalo litatumika kwa shughuli mbalimbali za walimu.
“Tunatoa
shukrani kwa Chama Cha Walimu Manispaa ya Shinyanga kwa kuiamini kampuni yetu
mama ya Dellah Car Traders Company. Tulikuwa Wazabuni watatu lakini sisi
tukashinda tenda ya kununua gari la CWT ambalo limegharimu jumla ya shilingi
milioni 49 na laki 9”,amesema Dellah.
Mtaalamu
huyo wa magari na Wakala wa uagizaji magari, amesema yupo tayari kutoa elimu
kuhusu namna ya kutunza gari hilo ili liwe imara zaidi na kuhakikisha linadumu
kwa muda mrefu huku akiongeza kuwa pia wamefunga TV na muziki wa kisasa katika
gari hilo ili kuwapa raha zaidi walimu wa Manispaa ya Shinyanga.
Akipokea
gari hilo, Mwenyekiti wa CWT mkoa wa Shinyanga, John Balele amesema gari hilo
ni zuri na injini yake ni nzuri akibainisha kuwa gari hilo siyo kwa ajili ya
viongozi wa CWT bali litatumika kwa ajili ya walimu wote bila ubaguzi wa aina
yoyote.
“Wengi
hawakuamini kama Dellah Car Traders
Company wangeleta gari zuri lakini ukweli ni kwamba wameleta gari zuri.
Tumefurahi gari tuliloagiza ndiyo gari waliloleta. Mchakato wa kununua gari
hili ulikuwa mgumu sana, tulikuwa na Wazabuni watatu. Tunawapongeza Dellah
kutuletea gari zuri. Dellah, kamati ya manunuzi na kamati tendaji ya CWT
mmetuheshimisha”,amesema Balele.
Aidha
ametumia fursa hiyo kuwataka walimu kutunza gari na kuepuka kutozozania gari
hilo na watengeneze kanuni za kuendeshea
gari hilo na kuhakikisha linatumika kwa shughuli za walimu siyo kwa malengo ya
biashara vinginevyo litawapa shida
Naye
Mwenyekiti wa CWT Manispaaa ya Shinyanga, Meshack Mashigala amesema gari hilo
litatumika kusaidia walimu katika shida
na raha akieleza kuwa walimu walikuwa wanapata changamoto kubwa ya usafiri
pindi wanapopatwa na matatizo.
“Pongezi
nyingi ziwafikie walimu wa Manispaa ya Shinyanga ambao wana mategemeo makubwa
katika gari hili ambapo sasa shida zao zitaisha”,amesema Mashigala.
Awali
akisoma taarifa ya ununuzi wa gari la CWT Manispaa ya Shinyanga, Katibu wa CWT
Manispaa ya Shinyanga, James Msimbang’ombe amesema waliingia mkataba na Kampuni
ya Dellah Car Traders Company kununua gari Novemba 25,2020 kwa gharama ya
shilingi milioni 49.9 ambapo Kampuni hiyo imeleta gari hilo ndani ya siku 45.
Muonekano wa gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ lenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga likiwa nje ya Ofisi za CWT mkoa wa Shinyanga baada ya kuletwa na Kampuni ya Uagizaji Magari ya Dellah Car Traders Company leo Ijumaa Februari 5,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu wa CWT Manispaa ya Shinyanga, James Msimbang’ombe akisoma taarifa ya ununuzi wa gari la CWT Manispaa ya Shinyanga, amesema waliingia mkataba na Kampuni ya Dellah Car Traders Company kununua gari Novemba 25,2020 kwa gharama ya shilingi milioni 49.9 ambapo Kampuni hiyo imeleta gari hilo ndani ya siku 45.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company inayojihusisha na uagizaji magari Japan, Dubai, Singapore na UK, Edwin Charles Dellah akikishukuru Chama Cha Walimu Manispaa ya Shinyanga kwa kuiamini Kampuni hiyo kuwaagizia gari Japan Desemba 16,2020 na gari hiyo imefika ndani ya siku 45 ambapo iliwasili Dar es salaam Januari 28, 2021 na wamekabidhi leo Februari 5,2021.
wenyekiti wa CWT Manispaaa ya Shinyanga, Meshack Mashigala akizungumza wakati wa kupokea gari hilo ambapo amesema gari hilo litatumika kusaidia walimu katika shida na raha akieleza kuwa walimu walikuwa wanapata changamoto kubwa ya usafiri pindi wanapopatwa na matatizo.
Mwenyekiti wa CWT mkoa wa Shinyanga, John Balele akizungumza wakati wa kupokea gari aina ya Toyota Coaster ambapo amesema gari hilo ni zuri na injini yake ni nzuri akibainisha kuwa gari hilo siyo kwa ajili ya viongozi wa CWT bali litatumika kwa ajili ya walimu wote bila ubaguzi wa aina yoyote.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company, Edwin Charles Dellah akielezea kuhusu usajili wa gari aina ya Toyota Coaster kwa ajili ya Chama Cha Walimu Manispaa ya Shinyanga wakati akikabidhi nyaraka za manunuzi ya gari.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company inayojihusisha na uagizaji magari Japan, Dubai, Singapore na UK, Edwin Charles Dellah akimkabidhi Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Shinyanga, Lazaro Saulo nyaraka za ununuzi wa gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ ikiwa na thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company inayojihusisha na uagizaji magari Japan, Dubai, Singapore na UK, Edwin Charles Dellah akimkabidhi Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Shinyanga, John Balele nyaraka za ununuzi wa gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ yenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Shinyanga, John Balele akiwakabidhi Viongozi wa CWT Manispaa ya Shinyanga nyaraka za ununuzi wa gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ yenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa CWT mkoa wa Shinyanga, John Balele akizindua gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ yenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa kulimwagia maji kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company akibandua kibao cha Dellah Car Traders Company ili kibao cha gari aina ya Coaster chenye namba za usajili T 682 DVJ kionekane.
Kibao cha gari aina ya Toyota Coaster kikionesha namba za usajili T 682 DVJ baada ya kibao cha Dellah Car Traders Company kubanduliwa.
Walimu na wafanyakazi wa Dellah Car Traders Company wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company inayojihusisha na uagizaji magari Japan, Dubai, Singapore na UK, Edwin Charles Dellah akiwasha muziki ndani ya gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ lenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga.
Baadhi ya walimu wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ yenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa CWT mkoa wa Shinyanga John Balele (kushoto) akimpongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company inayojihusisha na uagizaji magari Japan, Dubai, Singapore na UK, Edwin Charles Dellah kwa ununuzi wa gari nzuri aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ lenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga likiwa nje ya Ofisi za CWT mkoa wa Shinyanga baada ya kuletwa na Kampuni ya Uagizaji Magari ya Dellah Car Traders Company leo Ijumaa Februari 5,2021.
Shangwe zikitawala baada ya makabidhiano ya gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ lenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga nje ya Ofisi za CWT mkoa wa Shinyanga baada ya kuletwa na Kampuni ya Uagizaji Magari ya Dellah Car Traders Company leo Ijumaa Februari 5,2021.
Muonekano wa gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ lenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga
Wafanyakazi wa Dellah Car Traders Company wakipiga picha ya kumbukumbu baada ya kukabidhi gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ yenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Uagizaji Magari ya Dellah Car Traders Company na viongozi wa CWT wakipiga picha ya kumbukumbu
Awali gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ lenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga likiwa nje ya Ofisi za Kampuni ya Uagizaji Magari ya Dellah Car Traders Company leo Ijumaa Februari 5,2021.
Muonekano wa bango nje ya ofisi za Kampuni ya Uagizaji Magari ya Dellah Car Traders Company katika jengo la Seif Hotel Mjini Shinyanga.
Maandamano yakiendelea mjini Shinyanga wakati wa zoezi la makabidhiano ya gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ yenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga.
Maandamano yakiendelea mjini Shinyanga wakati wa zoezi la makabidhiano ya gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ yenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga.
Maandamano yakiendelea mjini Shinyanga wakati wa zoezi la makabidhiano ya gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ yenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga.
Maandamano yakiendelea mjini Shinyanga wakati wa zoezi la makabidhiano ya gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ yenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga.
Maandamano yakiendelea mjini Shinyanga wakati wa zoezi la makabidhiano ya gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ lenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga.
Maandamano yakiendelea mjini Shinyanga wakati wa zoezi la makabidhiano ya gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 682 DVJ lenye thamani ya shilingi milioni 49.9 kwa ajili ya Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga baada ya kuletwa na Kampuni ya Uagizaji Magari ya Dellah Car Traders Company leo Ijumaa Februari 5,2021.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin