Picha : MKURUGENZI WA VANSON MICROFINANCE CO. LTD ASHEREHEKEA VALENTINE’S DAY KWA KULA CHAKULA, KUMWAGA ZAWADI KWA WATOTO WENYE UALBINO BUHANGIJA


Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ akikabidhi mchele kilo 500 kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga akisherehekea Valentine's Day. Kulia ni Mwalimu Mlezi wa watoto hao, Mwashum Ismail.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ amesherehekea Sikukuu ya Valentine kwa kula chakula cha pamoja, kutoa zawadi ya mchele kilo 500,juisi,pipi,biskuti, nguo na vifaa vya shule kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.

Higini amefanya hafla hiyo leo Jumapili Februari 14,2021 ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Wapendanao duniani ‘Valentine’s Day’ akiwa ameambatana Mdau wa maendeleo Pendo Edward ambaye amesherehekea siku yake ya kuzaliwa ‘Birthday’  Februari 14, 2021 kwa kukata keki na kula na watoto wenye ualbino, wasioona na Viziwi waliopo katika kituo hicho cha Buhangija pamoja na kuwapa zawadi ya pipi,biskuti na juisi za Kampuni ya Jambo Food Products anakofanyia kazi.

Higini pia aliambatana na mdau mwingine wa Maendeleo Husna Mayuhana (Mwalimu wa shule ya Sekondari Mwasele) ambaye ametoa msaada wa nguo na viatu kwa watoto hao.

Akizungumza wakati wa kula chakula na kukabidhi zawadi kwa watoto hao, Higini Thomas ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinanance Co. Ltd inayojihusisha na masuala ya mikopo katika Manispaa ya Shinyanga amesema ameona ni vyema afike katika kituo cha Buhangija kusherehekea siku ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ akifurahi na watoto ambao wana Ualbino kama yeye alivyo.

“Nimekuja kufurahi na watoto kwa sababu leo ni siku ya wapendanao na nimekuwa na utaratibu wa kufika hapa mara kwa mara na kuwapatia chochote kile ninachopata ili kuwafariji na kuwaonesha upendo kwani wanajisikia faraja pale wanapotembelewa”,amesema Higini.

“Mimi ni mhusika mwenzao, tukija sisi wenye uhalisia watoto hawa wanapata faraja na kujituma zaidi katika masomo yao na kutokata tamaa. Naomba wadau wengine waje katika kituo hiki ili kuwapa faraja watoto na kuwasaidia kwa mahitaji mbalimbali waliyonayo”,ameongeza Higini.

Naye Mwalimu Mlezi wa watoto hao, Mwashum Ismail akizungumza kwa niaba na Mkuu wa kituo cha Buhangija amewashukuru wadau hao wa watoto kwa kuandaa chakula cha pamoja na watoto pamoja na misaada waliyotoa hivyo kuwaomba wadau wengine kutembelea watoto hao.

Nao watoto wameshukuru kwa msaada waliopatiwa na kusisitiza wadau kufika katika kituo hicho.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ akizungumza wakati akisherehekea Sikukuu ya Valentine kwa kula chakula cha pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangiji na kutoa zawadi ya mchele kilo 500, juisi, pipi, biskuti, nguo na vifaa vya shule kwa watoto hao leo Jumapili Februari 14,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ akizungumza wakati akisherehekea Sikukuu ya Valentine kwa kula chakula cha pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija na kutoa zawadi ya mchele kilo 500, juisi, pipi, biskuti, nguo na vifaa vya shule kwa watoto hao leo Jumapili Februari 14, 2021.
Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ akikabidhi mchele kilo 500 kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangiji Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Mwalimu Mlezi wa watoto hao, Mwashum Ismail
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ akikabidhi mchele kilo 500 kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga akisherehekea Valentine's Day. Kulia ni Mwalimu Mlezi wa watoto hao, Mwashum Ismail
Muonekano wa kilo 500 za mchele
Muonekano wa zawadi mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija
Muonekano wa zawadi mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija
Muonekano wa sehemu ya juisi
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ na wadau wakijiandaa kugawa juisi na soda kwa watoto
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ akigawa chakula kwa watoto
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ akigawa chakula kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Zoezi la kugawa chakula kwa watoto likiendelea
Zoezi la kugawa chakula na vinywaji kwa watoto likiendelea
Mdau wa Maendeleo Husna Mayuhana ambaye ametoa msaada wa nguo kwa watoto katika kituo cha Buhangija akimfungulia juisi mmoja wa watoto hao.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ akiangalia watoto wakila chakula baada ya kuwagawia
Wadau wakiendelea na zoezi la kugawa juisi
Watoto wakiendelea kuchukua chakula
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ akila chakula katika kituo cha Buhangija
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ akizungumza na watoto
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ akitoa zawadi ya madaftari kwa watoto hao
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ akitoa zawadi ya madaftari na rula kwa watoto hao
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ akipiga picha na watoto aliowapa zawadi kutokana na kufanya vizuri kwenye mitihani kwa kushika namba moja, mbili na tatu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ akiendelea kugawa zawadi ya kalamu kwa watoto hao
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ na wadau wakiendelea na zoezi la kugawa nguo kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga. Kushoto ni Mdau wa Maendeleo Husna Mayuhana ambaye ametoa msaada wa nguo kwa watoto katika kituo cha Buhangija.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ na wadau wakiendelea na zoezi la kugawa nguo kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga. Katikati ni Mdau wa Maendeleo Husna Mayuhana ambaye ametoa msaada wa nguo kwa watoto katika kituo cha Buhangija.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ na wadau wakiendelea na zoezi la kugawa nguo kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga
Zoezi la kugawa pipi kwa watoto likiendelea
Mdau wa maendeleo Pendo Edward (kulia) ambaye amesherehekea siku yake ya kuzaliwa ‘Birthday’ akigawa pipi za Kampuni ya Jambo Food Products ambako anafanyia kazi.
Mdau Abel Kaholwe akigawa juisi kwa watoto
Mdau wa Maendeleo Husna Mayuhana ambaye ametoa msaada wa nguo kwa watoto katika kituo cha Buhangija akigawa juisi kwa watoto hao
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ akigawa juisi kwa watoto.
Mdau wa maendeleo Pendo Edward (kulia) ambaye amesherehekea siku yake ya kuzaliwa ‘Birthday’ leo Februari 14,2021 akizungumza kabla ya kukata keki na kula na watoto wenye ualbino, wasioona na Viziwi waliopo katika kituo hicho cha Buhangija.
Muonekano wa keki ya mdau wa maendeleo Pendo Edward ambaye amesherehekea siku yake ya kuzaliwa ‘Birthday’ kwa kula na watoto wenye ualbino, wasioona na Viziwi waliopo katika kituo hicho cha Buhangija.
Mdau wa maendeleo Pendo Edward akikata keki kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ‘Birthday’ kwa kula na watoto wenye ualbino, wasioona na Viziwi waliopo katika kituo hicho cha Buhangija.
Mdau wa maendeleo Pendo Edward akikata keki na kula na watoto wenye ualbino, wasioona na Viziwi waliopo katika kituo hicho cha Buhangija.
Mdau wa maendeleo Pendo Edward ambaye amesherehekea siku yake ya kuzaliwa ‘Birthday’ akiwalisha keki watoto wenye ualbino, wasioona na Viziwi waliopo katika kituo hicho cha Buhangija.
Mdau wa maendeleo Pendo Edward ambaye amesherehekea siku yake ya kuzaliwa ‘Birthday’ akiwalisha keki watoto wenye ualbino, wasioona na Viziwi waliopo katika kituo hicho cha Buhangija.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanson Microfinance Company Limited Higini Thomas Mwacha ‘Digna’ akiwalisha keki watoto
Mdau wa maendeleo Pendo Edward ambaye amesherehekea siku yake ya kuzaliwa ‘Birthday’ akijiandaa kugonga Cheers na watoto wenye ualbino, wasioona na Viziwi waliopo katika kituo hicho cha Buhangija akisherehekea Birthday yake leo Februari 14,2021.
Mdau wa maendeleo Pendo Edward ambaye amesherehekea siku yake ya kuzaliwa ‘Birthday’ akigonga cheers na watoto wenye ualbino, wasioona na Viziwi waliopo katika kituo hicho cha Buhangija.
Wadau wakiwa katika kituo cha Buhangija
Wadau wakiwa katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija.

Picha na Kadama Malunde -  Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post