DAKTARI AJITOKEZA KUMSAIDIA MWANAMKE ALIYEGANDISHA NYWELE ZAKE KWA GUNDI KIMAKOSA


Dkt Michael Obeng ameripotiwa kusema kuwa atatoa matibabu ya bure

Dkt Michael Obeng, Daktari bingwa wa upasuaji wa kurekebisha mwili, Mmarekani mwenye asili ya Ghana, amejitolea kumsaidia mwanamke ambaye hadithi yake ya kuweka gundi katika nywele zake iliwatia huruma wengi kwenye mtandao, kimeripoti kituo cha Televisheni cha a CBSN Los Angeles.

Tessica Brown alishirikisha umma video katika TikTok wiki iliyopita akisema alitumia gundi aina ya Gorilla Glue badala ya kujipulizia mafuta (hairspray) kushikilia nywele zake ziwe na mtindo alioutaka

Kwa kawaida gundi hiyo aliyoitumiwa ambayo haiyeyushwi na maji, hutumiwa kuweka sakafu za bafuni na sakafu za mbao.
Taarifa kuhusu mkasa wa nywele uliompata Tessica Brown, ulifahamika mapema mwezi Februari baada ya kusema kuwa amekuwa akiweka mtindo mmoja wa nywele kwa muda wa mwezi mmoja bila kubadili kwasababu alijpaka gundi badala ya mafuta na jitihada zake za kuosha nywele ziligonga mwamba.

"Nywele zangu haziwezi kuchanika au hata kuvutika.Nimeosha nywele zaidi ya mara 15 lakini hakuna mafanikio yoyote ziko vilevile." alisema kwenye mtandao wake wa Instagram.

Katika video Bi Brown alisema masaibu yake yalianza karibu mwezi mmoja uliopita na kwamba alijaribu vitu kadhaa kuondoa gundi iliyoganda kichwani havikufanikiwa:

Ukigundua kuwa huu ulikua ni ukweli I, unaweza kuhisi kumhurumia Tessica," Dkt Obeng aliiambia Televisheni ya CBSN.

"Tunataangalia dalili za vidonda vya kemikali, na tuna dawa ya kuzuia kuungua kama tukipata ziko...Matibabu haya yatafanyika baada ya kumchoma sindano ya usingizi ili asiweze kuhisi maumivu kabisa ," aliongeza.

Daktari huyo wa kurekebisha maumbile ya mwilialisemaaliwasiliana na Bi Tessica na alikuwa anapanga kuiondoa gundi, na kuokoa nywele yake, kwa matibabu ya kemikali maalumu.

Daktari huyo aliyepata mafunzo katika Chuo Kikuu cha Harvard , anayefanyia kazi katika Beverly Hills-alisema pia kuwa atamfanyia matibabu ambayo kwa kawaida hugharimu dola $12,000 (£8,000), kwa bure, iliripoti CBSN.

Dkt Obeng ambaye ni daktari bingwa wa upasuaji wa kurekebisha maumbile ya mwili na kulingana na wavuti wake ni muasisi wa wakfu unaosaidia kurekebisha muonekano wa watu kutoka nchi zinazoendela ili kuwarejeshea uthabiti wa hisia zao, wakfu unaotoa huduma bure.

Kampuni iliyotengeneza gundi ilisema nini?

Kwa mujibu wa tovuti ya Gorilla Glue , wameandika gundi ambayo aliitumia haiwezi kutoka kwa maji kwa asilimia 100% na matumizi yake ni kugundisha marumaru za bafuni na paa.

Kampuni hiyo iliposikia mkasa uliomkuta mwanamke huyo walimtumia ujumbe kwenye Twitter wakimuomba radhi kwa kile kilichomtokea.

Gorilla Glue imemwambia Bi Tessica kuwa kesi yake ni ya kipekee maana bidhaa yao si ya kuweka kwenye nywele hivyo wanadhani hakuna kitu anachoweza kukifanya kubadili hali iliyomkuta.

Kampuni hiyo ilimpa pole kwa kukutwa na tukio hilo na wanamtakia kila la kheri katika matibabu yake.

Walisema hawana cha kusema bali kumpa pole na hawashauri mtu yeyote kutumia bidhaa yao kwenye nywele. Na kama mtu akitumia na kujaribu kuziosha kwa sabuni au pombe anaweza kupata madhara mengine.

Gorilla Glue iliandika kabisa kuwa si kwa matumizi ya nywele.

Maelezo ya onyo katika bidhaa zao ni muhimu sana na wateja wanapaswa kuzingatia suala hilo.

Gundi yao ni kwa ajili ya kugundisha vitu kama makaratasi ,mbao, nguo lakini si nywele.

Juhudi za kujiokoa

Kwa mujibu wa taarifa ya TMZ , imeeleza kuwa kampuni ya Gorilla Glue ni kama dada huyo ataenelea kuishi wakati nywele zikiwa zimegundika na hakuna suluhu la tatizo lake , wamesema hata akienda mahakamani hana kesi ya kuwashitaki.


Mmoja wa wanafamilia ameeleza bado Bi.Brown anaendelea kupata matibabu.

Tessica tayari aalikwishaanza kuomba msaada na kuchangisha pesa za garama ya hospitali ... Mpaka sasa amepokea dola $9,000 kwa ajili ya matibabu na watu bado wanatuma.

 CHANZO - BBC SWAHILI

Soma pia:

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post