Aron Kagurumjuli
Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Aron Kagurumjuli na kwamba uteuzi wa mkurugenzi mwingine wa manispaa hiyo utafanywa baadaye.
Kagurumjuli aliteuliwa na Magufuli Julai 7, 2016 siku ambayo kiongozi huyo aliteua wakurugenzi wa halmashauri za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22 na Wilaya 137 za Tanzania Bara.
Social Plugin