Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Saidi Ahmed Bwanga akiwa ameshikilia bima za afya za ajili ya watoto 172 wenye mahitaji maalumu katika Manispaa ya Shinyanga zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Diwani wa
Kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga Mhe. Ezekiel John Sabo amefanya hafla
ya kula chakula cha pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu na wananchi wote wa
kata ya Ibinzamata ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa
diwani katika uchaguzi Mkuu mwaka 2020.
Hafla hiyo
iliyofanyika Jumapili Februari 7,2021 imeenda sambamba na maadhimisho ya miaka
44 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kata ya Ibinzamata ambapo mgeni rasmi
alikuwa Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Saidi Ahmed Bwanga.
Sabo amesema
ameamua kula chakula cha pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha
Buhangija ili kuwaonesha upendo watoto hao lakini kula chakula na wananchi wa
kata ya Ibinzamata ili kuwashukuru kwa kumchagua kuwa diwani wao na kuchagua
mbunge Patrobas Katambi na Rais John Pombe Magufuli katika uchaguzi mkuu 2020.
“Ninakipongeza
Chama cha Mapinduzi kwa ushindi mnono katika uchaguzi mkuu 2020.Nawashukuru na
kuwapongeza walimu na walezi wa watoto wenye mahitaji maalumu jinsi
wanavyojitolea kuhudumia watoto hawa vizuri”,amesema Sabo.
Akizungumza
katika sherehe hizo, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga
Mjini, Said Bwanga amemshukuru na kumpongeza Diwani wa kata ya Ibinzamata Ezekiel John Sabo kwa kuandaa sherehe hizo na
kueleza kuwa CCM kudumisha amani na ushirikiano.
“Tunaposherehekea
miaka 44 ya CCM tuna kila sababu ya kutembea kifua mbele kujivunia mafanikio tuliyofikia.
Tunaendelea kujivunia amani na upendo hivyo tuwaepuke baadhi ya watu
wanaotumiwa na Mabeberu kuharibu sifa ya nchi yetu”,amesema Bwanga.
Katika hatua
nyingine amewataka Madiwani, Maafisa Watendaji na baadhi ya viongozi
wanaolazimisha wananchi kuchangia ujenzi wa shule, madarasa na madawati kwa
lazima na walimu kutowarudisha nyumbani wanafunzi ambao hawajatoa michango bali
wananchi wanatakiwa kuelimishwa ili wachangie kwa hiari.
Katika
sherehe hizo, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi ametoa
msaada wa Bima za Afya za CHF iliyoboreshwa kwa watoto 272 wenye uhitaji
maalumu kutoka vituo vitatu ambavyo ni Buhangija kinacholea watoto wenye
ualbino,wasioona na Viziwi 231, kituo cha watoto wenye utindio wa ubongo cha
Kitangiri watoto 21 na kituo cha Bushushu kata ya Lubaga watoto 20.
Bima hizo za afya kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu zimekabidhiwa na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samwel Jackson akimwakilisha Mbunge Patrobas Katambi ambaye yupo Jijini Dodoma akiendelea na majukumu mengine.
Naye Mkurugenzi
wa Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd Gilitu Nilla Makula ametoa msaada wa
Televisheni (Flat Screen) na Dish Dish la Azam katika kituo cha kulelea watoto cha
Buhangija kwa ajili ya kuangalia taarifa mbalimbali.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Saidi Ahmed Bwanga akizungumza wa hafla ya Diwani wa Kata ya Ibinzamata Ezekiel John Sabo kula chakula cha pamoja wananchi na watoto wenye mahitaji maalumu katika Kituo cha Buhangija kilichopo katika kata ya Ibinzamata sambamba na maadhimisho ya Miaka 44 ya Chama Cha Mapinduzi Jumapili Februari 7,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Saidi Ahmed Bwanga akizungumza wa hafla ya Diwani wa Kata ya Ibinzamata Ezekiel John Sabo kula chakula cha pamoja wananchi na watoto wenye mahitaji maalumu katika Kituo cha Buhangija kilichopo katika kata ya Ibinzamata sambamba na maadhimisho ya Miaka 44 ya Chama Cha Mapinduzi Jumapili Februari 7,2021.
Diwani wa Kata ya Ibinzamata Ezekiel John Sabo akizungumza wakati wa hafla aliyoiandaa kwa ajili ya kula chakula cha pamoja wananchi na watoto wenye mahitaji maalumu katika Kituo cha Buhangija kilichopo katika kata ya Ibinzamata sambamba na maadhimisho ya Miaka 44 ya Chama Cha Mapinduzi Jumapili Februari 7,2021.

Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Samwel Jackson akielezea kuhusu Bima za Afya za CHF iliyoboreshwa zilitolewa na Mbunge Patrobas Katambi kwa watoto 272 wenye uhitaji maalumu kutoka vituo vitatu ambavyo ni Buhangija kinacholea watoto wenye ualbino,wasioona na Viziwi 231, kituo cha watoto wenye utindio wa ubongo cha Kitangiri watoto 21 na kituo cha Bushushu kata ya Lubaga watoto 20.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi, Bw. Samwel Jackson akionesha Bima za Afya za CHF iliyoboreshwa kwa watoto 272 wenye uhitaji maalumu zilizotolewa na Mbunge Patrobas Katambi.
Sehemu ya Bima za Afya za CHF iliyoboreshwa kwa watoto 272 wenye uhitaji maalumu zilizotolewa na Mbunge Patrobas Katambi.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi, Bw. Samwel Jackson akimkabidhi Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Saidi Bwanga (kulia) Bima za Afya za CHF iliyoboreshwa kwa watoto 272 wenye uhitaji maalumu zilizotolewa na Mbunge Patrobas Katambi.

Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Saidi Ahmed Bwanga akiwakabidhi watoto bima za afya ambazo ni sehemu ya kadi za bima ya afya kwa ajili ya watoto 272 wenye mahitaji maalumu katika Manispaa ya Shinyanga zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Saidi Ahmed Bwanga akimkabidhi mtoto bima ya afya ambayo ni sehemu ya kadi za bima ya afya kwa ajili ya watoto 272 wenye mahitaji maalumu katika Manispaa ya Shinyanga zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd Gilitu Nilla Makula akizungumza wakati wa sherehe hizo ambapo ametoa msaada wa Televisheni (Flat Screen) na Dish Dish la Azam katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija kwa ajili ya kuangalia taarifa mbalimbali.
Mwenyekiti wa kamati ya chakula kwenye hafla ya chakula pamoja maadhimisho ya miaka 44 ya CCM, Teddy Shaban ambaye alikuwa Meneja Kampeni wa Diwani Ezekiel John Sabo akizungumza wakati hafla hiyo.
Afisa Mtendaji wa kata ya Ibinzamata Victor Kajuna akizungumza kwenye hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Dotto Joshua akizungumza wakati wa sherehe hizo
Katibu wa UVCCM mkoa wa Shinyanga, Muhsin Zikatim akizungumza kwenye sherehe hizo
Kaimu Katibu
CCM Kata ya Ibinzamata ambaye ni Katibu wa Siasa na Uenezi kata ya Ibinzamata Ibrahim
Abdallah akizungumza wakati wa sherehe hizo
Mwenyekiti wa CCM kata ya Ibinzamata, Haruna Seleman Mkuki akizungumza kwenye sherehe hizo
Watoto wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Watoto wakiwa eneo la tukio
Watoto wakiwa katika eneo la tukio
Sherehe zikiendelea
Sherehe zikiendelea
Sherehe zikiendelea
Mabago Ibrahim akisoma risala kwa niaba ya Katibu wa CCM kata ya Ibinzamata
Wananchi na wachama wa CCM wakiwa kwenye sherehe
Kamati ya chakula wakijiandaa kugawa chakula kwa watoto na wananchi wa kata ya Ibinzamata.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com