Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ameongoza mapokezi ya mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John William Kijazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA). Mwili wa marehemu Balozi Kijazi utaagwa kesho Ijumaa Februari 19, 2021 katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam na kisha kusafirishwa kwenda Wilayani Korogwe, Tanga kwa ajili ya mazishi.
Social Plugin