Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI WA MAJI AAHIDI NEEMA YA MAJI KIJIJI CHA KASENGA

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi. Maryprisca Mahundi (Mb) amewataka wananchi wa kijiji cha Kasenga wilaya ya Chato mkoani Geita kutunza miundombinu ya maji ili iwe endelevu kwa vizazi vijavyo. 

Ameongea hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kasenga  waliosimamisha msafara wake ili waweze kuishukuru serikali kwa kuwajali kwa kuwakarabatia miundombinu ya mradi wao wa maji ambao uliacha kutoa maji tangu mwaka 1988.

“Tunafahamu mlikuwa na mradi wa siku nyingi ambao muda mrefu ulikuwa hautoi maji lakini sasa mradi umefufuliwa na umeanza kutoa maji, tunafahamu vituo vitatu vimeanza kutoa maji na baadhi ya maeneo bado hawajaanza kupata huduma hiyo, Nataka kuwahakikishia hivi vituo ambavyo havijapatiwa huduma ya maji baada ya mwezi mmoja vitapata maji”, amesema Mhandisi Mahundi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com