Mwili wa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad utazikwa kesho Alhamisi Februari 18, 2021 mjini Pemba, Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaeleza kuwa mwili wa mwenyekiti huyo wa chama cha ACT-Wazalendo aliyefariki dunia leo saa 5 asubuhi katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) utaondoka na ndege kesho asubuhi kwenda mjini Unguja ambako itafanyika sala katika viwanja wa Mnazi Mmoja.
Inaeleza kuwa saa 6 mchana utasafirishwa kwenda Pemba na sala itafanyika katika viwanja vya Gombani na kisha safari ya kueleka Mtambwe kwa mazishi yatakayofanyika saa 10 jioni itaanza.
Social Plugin