Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AFARIKI DUNIA


Andrew Mollel enzi za uhai wake

Na Mussa Juma - Arusha
 Mfanyabiashara maarufu mkoani Arusha, Andrew Mollel ambaye alikuwa mwanzilishi na Mkurugenzi wa kampuni mbalimbali mkoani Arusha amefariki dunia na kuibua simanzi kwa wakazi wengi wa jiji hilo.

Akizungumza na Mwananchi leo, Februari 28, Mbunge wa jimbo la Monduli , Fredrick Lowassa amesema kifo cha Mollel ni pigo kubwa katika jiji la Arusha kutokana na mchango wake.

Lowassa amesema taratibu za mazishi wa Mollel zinaendelea kufanywa na wanafamilia lakini, kubwa ambalo Arusha watamkumbuka ni kuandaa michoro ya mradi mkubwa wa nyumba za PPF zilizopo eneo la Kijenge jijini hapa ambalo lilikuwa ni eneo lake.

Mollel alikuwa pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Happy Sausages ,Kijenge Animal Products Limited, Georges Center Ltd na AGM Holding na pia mjumbe wa bodi mbalimbali hapa nchini.

Via Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com