Halmashauri Kuu ya Kanisa la KKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria imefanya hafla fupi ya kuwapongeza wanafunzi wa shule ya sekondari Mwadui inayomilikiwa na Kanisa hilo kwa kufanya vizuri katika masomo yao.
Katika hafla hiyo imefanyika Februari 17,2021 ikiongozwa na Askofu wa Kanisa la KKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dkt. Emmanuel Makala na kuhudhuriwa na msaidizi wa Askofu Mchungaji Yohana Ernest Nzelu,viongozi mbalimbali wa Kanisa, wachungaji, baadhi ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya Dayosisi, Walimu na watendaji wa shule wasio walimu pamoja na wanafunzi imefanyika katika ukumbi wa REDEEMER ulioko katika Shule ya Sekondari Mwadui.
Akizungumza katika hafla hiyo, Askofu Dkt. Emmanuel Makala amesema Dayosisi imepokea ombi la serikali lililotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu kwa niaba ya mkuu wa mkoa kujenga Chuo Kikuu na kueleza kuwa inawezekana hata shule hiyo ya Mwadui Sekondari ikabadilishwa na kuwa Chuo Kikuu.
Hata hivyo amempongeza Mkuu wa shule hiyo Mchungaji Yohana Ernest Nzelu ambaye ndiye msaidizi wa Askofu na kuweka wazi kuwa ataendelea kuwa mkuu wa Shule hadi mabadiliko yatakapofanyika.
Pia ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wanafunzi wa shule hiyo kwa kufanya vizuri mitihani yao ya kuhitimu na kufaulu vizuri pia amewatia moyo walimu na watumishi wengine wa shule hiyo kwa kazi nzuri wanayofanya.
Hata hivyo Askofu Dkt. Makala hakusita kuwakumbusha waumini na wananchi kwa ujumla kuendekea kuchukua tahadhari ya Corona pamoja na magonjwa mengine ya kuambukiza lakini pia amekumbusha umuhimu wa kufanya mazoezi kama njia pekee ya kupiga vita baadhi ya magonjwa.
Naye Msaidizi wa Kanisa la KKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Mchungaji Yohana Ernest Nzelu ambaye ni Mkuu wa shule ya Sekondari Mwadui ametoa wito kwa walimu kuendelea kufanya bidii kufundisha kwa weledi na kujituma ambapo amesema uongozi wa shule umelazimika kufumua idara ya masomo ya Sayansi kwakuwa licha ya wanafunzi kufaulu vizuri katika mitihani ufaulu wa masomo hayo haukuwa mzuri hivyo ni wajibu wake na viongozi wengine wakiwamo walimu kutafuta njia ya kutatua hali hiyo.
Aidha ameupongeza Usharika wa Mwadui kwa kuwa mstari wa mbele na msaada mkubwa kwa mambo mengi na katika changamoto mbalimbali zinazojitokeza shuleni hapo.
Pia amezungumzia mpango wa kuanzisha kituo cha Watoto yatima kuwa bado unaendelea na taratibu za usajili unaendelea huku akiainisha mpango wa ujenzi wa kujenga nyumba za watendakazi wa shule na kueleza kuwa kazi hiyo itaanza punde kazi ya ujenzi wa fensi ya eneo la shule utakapokamikika.
Mkuu wa Shule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu ambaye ni msaidizi wa Baba Askofu Emmanuel Makala amesema kwamba amefurahishwa na wanafunzi wa shule hiyo kujituma si kwa upande wa masomo tu bali hata katika kumtumikia mungu kwa njia ya nyimbo na ibada na kuahidi kuwanunulia System mpya ya Muziki ambayo ataikabidhi siku chache zijazo.
Aidha Mchungaji Yohana Ernest Nzelu amesema amepokea kwa mikono miwili utume mpya Kama msaidizi wa Askofu na kuwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu pamoja na halmashauri kuu ya Dayosisi chini ya uongozi wa Askofu Dkt. Emmanuel Makala kumteua Kuwa msaidizi wa Askofu.
Askofu wa Kanisa la KKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dkt. Emmanuel Makala akizungumza
Msaidizi wa Kanisa la KKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Mchungaji Yohana Ernest Nzelu ambaye ni Mkuu wa shule ya Sekondari Mwadui akizungumza
Msaidizi wa Kanisa la KKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Mchungaji Yohana Ernest Nzelu ambaye ni Mkuu wa shule ya Sekondari Mwadui akizungumza