Siku za karibuni kumekuwapo na matangazo yanayonadi pipi hizo maarufu kama ‘pipi mahaba’ ambazo pia zinauzwa kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya wanawake, zikiwamo saluni.
Mamlaka za Serikali, ikiwamo Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Baraza la Tiba Asili na Tiba mbadala na taasisi hizi zote zimeeleza kutozifahamu pipi hizo wala zinavyotengenezwa.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Mwananchi hivi karibuni umebaini kuwa wanawake wanazichangamkia pipi hizo zinazodaiwa kusaidia kuongeza uwezo, hamu ya kushiriki tendo la ndoa na kumfurahisha mwanaume.
Pipi hizo zenye rangi nyeupe mithili ya maji zimekuwa habari ya mjini kwa sasa, kuanzia mitandaoni hadi katika maeneo yenye mikusanyiko ya wanawake.
Kulingana na wauzaji, pipi hizo ni suluhisho la matatizo ya kimwili yanayoweza kumletea vikwazo mwanamke katika ushiriki wake kwenye tendo la ndoa.
Via Mwananchi
Social Plugin