Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KATIBU TAWALA MKOA WA ARUSHA AFARIKI DUNIA AJALI YA BASI NA GARI ALILOPANDA


Katibu tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega enzi za uhai wake

Na Mussa Juma - Mwananchi

 Katibu tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega amefariki dunia katika ajali ya gari leo Jumatano Februari 3, 2021 wakati akitoka mkoani humo kwenda Dodoma baada ya gari alilokuwa amepanda kugongana na basi.

Akizungumza na Mwananchi Digital mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti amesema ajali hiyo imetokea eneo la Mdori Mizani.

Amesema katika ajali hiyo watu wengine wanne wamejeruhiwa ambao ni dereva wa katibu tawala huyo na wanawake watatu waliokuwa kwenye basi.

"Ni ajali mbaya kumpoteza katibu tawala na muda huu tunajiandaa kurejesha mwili Arusha bado tupo kituo cha afya hapa Magugu,” amesema.

Amesema majeruhi wanaendelea vizuri na wamehamishiwa hospitali ya Mkoa wa Manyara.

Basi lililogongana na gari la katibu tawala huyo lilikuwa linatoka Singida kwenda Arusha.

Leo asubuhi Kwitema alimwakilisha katibu mkuu wa Wizara ya Fedha, Dotto James kwenye mkutano wa wizara hiyo na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu uboreshaji wa mfumo wa kielektroniki wa malipo serikalini (GePG) uliofanyika mjini Arusha.

CHANZO- MWANANCHI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com