Bodi ya Zabuni ya Mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA), ikikagua utekelezaji wa miradi ya maji ambayo ya Wakala wa Maji Vijiji (RUWASA) ambayo hua wanaiidhinishia fedha za utekelezaji wa miradi hiyo, kushoto ni Meneja Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) mkoani Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela akiwa na bodi hiyo.
Na Marco Maduhu, Shinyanga.
Bodi ya Zabuni (Tender board) ya Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA), ambayo ina husika pia kuidhinisha fedha za manunuzi vifaa vya utekelezaji miradi ya maji ambayo inatekelezwa na wakala wa maji vijijini (RUWASA) mkoani Shinyanga, imeridhishwa na ujenzi wa miradi hiyo ya maji vijijini.
Bodi hiyo ilianza ziara Februari 12,2021 kutembelea utekelezaji wa miradi hiyo ya maji ambayo ina tekelezwa na (RUWASA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Manispaa na Ushetu Manispaa ya Kahama, na kuhitimishwa jana, ambapo jumla ya miradi 12 imekaguliwa yenye thamani ya Sh. Bilioni 5.2 ambayo yote ipo kwenye hatua ya umaliziaji na mingine imeanza kutoa maji.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya Zabuni Rubeni Mwandubya, akizungumza mara baada ya kuhitimisha kukagua utekelezaji wa miradi hiyo ya maji, amesema wameridhishwa na miradi hiyo, ambapo mingi ipo kwenye hatua ya ukamilishaji na baadhi imeanza kutoa huduma ya maji.
Amesema miradi yote ambayo wameitembelea imeshakamilika kwa asilimia 90, na kuna vitu bado vinakamilishwa ili wakabidhiwe wananchi na kuanza kuchota maji, ambapo baadhi yake ipo kwenye usafishaji wa njia za mabomba na inatoa maji, jambo ambalo amebainisha kufurahishwa nalo, sababu ya kutekelezwa kwa wakati na kuwaondolea wananchi adha ya kutumia maji yasiyofaa kiafya.
“Lengo la ziara yetu ni kukagua kuona miradi ambayo hua tuna idhinisha fedha zake je ipo inatekelezwa na inaendana na thamani halisi ya fedha, na baada ya kuiona miradi hii, Bodi ya Zabuni tumeridhishwa na miradi yote ambayo inatekelezwa na (RUWASA), kiukweli wamefanya vizuri sababu miradi ipo kwenye hatua ya ukamilishaji na mingine inatoa maji,”amesema Mwandubya.
“Tunachosisitiza tu kwa RUWASA, waikamilishe miradi hii kwa muda ambao umepangwa, ili waikabizi kwa wananchi na kuanza kuchota maji safi na salama, na kuondokana na changamoto ya kupoteza muda mrefu kutafuta maji salama, na kutotumie tena maji yasiyofaa kwa afya zao,”ameongeza.
Kwa upande wake Meneja Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA),mkoani Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela, amesema miradi yote 12 ya maji safi na salama ambayo wanaitekeleza katika jijiji 20 vita hudumia wananchi zaidi ya 70,000, ambapo hadi kufikia mwezi March mwaka huu itakuwa imekamilika kwa asilimia 100.
Aidha amesema (RUWASA) katika mwaka wa fedha (2020-2021) walitenga kiasi cha fedha Sh, Bilioni 12, kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maji safi na salama maeneo ya vijiji, ambapo lengo la Serikali hadi kufikia (2025) huduma ya maji katika maeneo yote ya vijijini iwe imeshakamilika kwa asilimia 85.
Nao baadhi ya wananchi ambao ni wanufaika na miradi hiyo ya maji safi na salama akiwamo Aziza Joseph mkazi wa kijiji cha Masengwa, na Mary Daudi kijiji cha Ng’wang’osha wilayani Shinyanga, wameishukuru RUWASA kwa kuwatekelezea miradi hiyo ya maji vijijini, ambayo itawaondolea adha ya ukosefu wa maji kijijini na kuacha kutumia maji yasiyofaa kwa afya zao.
Pia wanafunzi wa shule ya Sekondari Masengwa, wamesema mradi wa maji safi na salama shuleni hapo utakuwa mkombozi kwao, kwa kuondokana na kufuata maji umbari mrefu na kupoteza vipindi vya masomo, pamoja na kuwaepusha na vishawishi vya kutongozwa na wanakijiji na kujikuta wengine wakiambulia ujauzito na kukatisha masomo.
Eta Elisoni ambaye ni mwanafunzi anayesoma kidato cha tatu katika shule hiyo ya Masengwa, anasema katika shule hiyo wanafunzi wa kike hua wanakaa Hostel, lakini changamoto ambayo inawakabili ni kufuata maji umbari wa kilomita moja na kuwafanya kukuatana na vishawishi njiani vya kutongozwa.
"Wanafunzi wa kike ambao tuanaishi Hostel hapa Shuleni, hua tunakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji, na tunapofuata maji kijiji jirani cha Mwamatongo, hukumbana na vishawishi vya kutongozwa kila siku, na baadhi yetu hupata ujauzito na kuacha masomo lakini kuanza kwa mradi huu wa maji safi na salama hapa shule changamoto hii itakwisha kabisa na hatimaye kutimiza ndoto zetu" amesema Elisoni.
Naye Mkuu wa Shule hiyo ya Sekondari Masengwa Salu Mlyambate, amesema Changamoto hiyo ya ukosefu wa maji shuleni hapo, imekuwa kikwazo kitaaluma kwa wanafunzi wa kike ambao wanaishi Hostel, sababu ya kupoteza muda wa Masomo kutokana na kufuata maji, na wengine kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanakijiji.
Aidha amesema mradi huo wa maji itakuwa mkombozi mkubwa na hatimate wanafunzi hao kuongeza ufaulu kwenye mitihani yao ya kuhitimu kidato cha Nne, ambapo pia wamekuwa wakifanya vizuri, na kutaja katika matokeo ya mwaka jana wanafunzi waliopata daraja la kwanza walikuwa ni wasichana wote watatu.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni Rubeni Mwandubya, akizungumza mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua miradi ya maji ambayo inatekelezwa na Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) mkoani Shinyanga.
Meneja Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) mkoani Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela, akielezea namna wanavyotekeleza miradi ya maji vijijini na kuhakikisha wana mtua ndoo kichwani Mwanamke.
Aziza Joseph mkazi wa kijiji cha Masengwa, akielezea namna wanavyopata adha kutokana na ukosefu wa maji safi na salama kijijini humo, pamoja na ujio wa mradi huo wa maji ambao utakuwa mkombozi kwao.
Maria Robert mkazi wa kijiji cha Uzogore, akielezea namna mradi wa maji safi na salama, ulivyo wakomboa wanawake kijijini hapo sababu ya kufuata maji umbari mrefu.
Mwanafunzi Eta Elisoni anayesoma katika Shule ya Sekondari Masengwa, akielezea namna mradi huo wa maji safi na salama kufika shuleni hapo utakavyo wasaidia wanafunzi kuondokana na changamoto na kufuata maji umbari mrefu na kukumbana na vishawishi vya kutongozwa.
Bodi ya Zabuni ikikagua mradi wa maji katika kijiji cha Ihapa ambao unatekelezwa na RUWASA.
Ukaguzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Ihapa ukiendelea.
Ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Uzogore ukiendelea.
Ukaguzi wa kituo cha kuchotea maji( BP) katika Shule ya Sekondari Masengwa wilyani Shinyanga ukiendelea.
Meneja Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) mkoani Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela, akikagua kituo cha kuchotea maji katika kijiji cha Masengwa wilayani Shinyanga.
Ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Ng'wang'osha ukiendelea.
Ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Azimio wilayani Shinyanga.
Ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Mwabomba Halmashauri ya Ushetu Manispaa ya Kahama, ukiendelea.
Ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Igwamanoni Halmashauri ya Ushetu Manispaa ya Kahama.
Awali Meneja Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA)mkoani Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela, akikagua ujenzi wa Tenki la kupozea kasi ya maji, katika kijiji cha Masengwa wilayani Shinyanga.
ukaguzi wa ujenzi wa Tenki la maji ukiendelea.
Ukaguzi wa Tenki la kuhifadhia maji katika kijiji cha Ibubu wilayani Shinyanga.
ukaguzi ukiendelea.
Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni Rubeni Mwandubya, akikagua mabomba ya maji, kwenye Tenki la kuhifadhia maji la mradi wa kijiji cha Ibubu wilayani Shinyanga.
Matengenezo ya bomba la maji katika kijiji cha Mwang'haranga ukiendelea, wilayani Shinyanga.
Awali Bodi ya Zabuni ikiwa katika ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Mwabomba Halmashauri ya Ushetu Manispaa ya Kahama.
Ukaguzi ukiendelea wa utekelezaji wa mradi wa maji safi na salama katika kijiji hicho cha Mwabomba Halmashauri ya Ushetu Manispaa ya Kahama.
ukaguzi ukiendelea.
Tenki la kuhifadhia maji katika mradi wa kijiji cha Mwabomba Halmashauri ya Ushetu Manispaa ya Kahama.
Ukaguzi wa Tenki la kuhifadhia maji safi na salama katika kijiji cha Ingwamanoni Halmashauri ya Ushetu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.
Awali ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji ikiendelea.
Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumaliza kukagua utekelezaji wa miradi ya maji ya RUWASA.
Na Marco Maduhu- Shinyanga.